2 Chronicles 30:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walichukua nafasi zao hekaluni kulingana na maagizo yaliyokuwamo katika sheria za Mose, mtu wa Mungu. Walawi waliwapa makuhani damu ya tambiko, nao wakainyunyiza madhabahuni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha wakachukua nafasi zao za kawaida kama ilivyoelezwa katika Torati ya Musa mtu wa Mungu. Makuhani wakanyunyiza ile damu waliyokabidhiwa na Walawi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakasimama mahali pao kwa taratibu yao, sawasawa na torati ya Musa, mtu wa Mungu; nao makuhani wakainyunyiza damu, waliyoipokea mikononi mwa Walawi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walichukua nafasi zao hekaluni kulingana na maagizo yaliyokuwamo katika sheria za Mose, mtu wa Mungu. Walawi waliwapa makuhani damu ya tambiko, nao wakainyunyiza madhabahuni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha wakachukua nafasi zao za kawaida kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Mose mtu wa Mungu. Makuhani wakanyunyiza ile damu waliyokabidhiwa na Walawi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha wakachukua nafasi zao za kawaida kama ilivyoelezwa katika Torati ya Musa mtu wa Mungu. Makuhani wakanyunyiza ile damu waliyokabidhiwa na Walawi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakasimama mahali pao kwa taratibu yao, kulingana na Torati ya Musa, mtu wa Mungu; nao makuhani wakainyunyiza damu, waliyoipokea mikononi mwa Walawi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walichukua nafasi zao hekaluni kulingana na maagizo yaliyokuwamo katika sheria za Mose, mtu wa Mungu. Walawi waliwapa makuhani damu ya tambiko, nao wakainyunyiza madhabahuni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakasimama mahali pao palipowapasa, kama Maonyo ya Mose aliyekuwa mtu wa Mungu yalivyoagiza. Hao watambikaji wakazinyunyiza damu, walizozipokea mikononi mwa Walawi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakasimama mahali pao kwa taratibu yao, sawasawa na torati ya Musa, mtu wa Mungu; nao makuhani wakainyunyiza damu, waliyoipokea mikononi mwa Walawi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakatwaa nafasi zao katika hekalu kulingana na maagizo yaliyokuwa katika Sheria ya Musa, mutu wa Mungu. Walawi wakawapa makuhani damu ya sadaka, nao wakainyunyiza juu ya mazabahu.