2 Chronicles 30:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa vile wengi wa wale waliokusanyika hapo hawakuwa wamejitakasa, iliwabidi Walawi kuwachinjia wanakondoo wa Pasaka na kuwaweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa wengi waliokuwa katika lile kusanyiko walikuwa hawajajitakasa, iliwapasa Walawi wachinje wana-kondoo wengine wa Pasaka kwa ajili ya wale watu ambao hawakuwa wametakaswa, ili kuwatakasa kwa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana kulikuwa na wengi katika kusanyiko ambao hawajajitakasa; kwa hiyo Walawi wakamchinjia pasaka, kila mtu asiyekuwa safi, ili kuwatakasa kwa Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa vile wengi wa wale waliokusanyika hapo hawakuwa wamejitakasa, iliwabidi Walawi kuwachinjia wanakondoo wa Pasaka na kuwaweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa wengi waliokuwa katika lile kusanyiko walikuwa hawajajitakasa, iliwapasa Walawi wachinje wana-kondoo wengine wa Pasaka kwa ajili ya wale watu ambao hawakuwa safi, kwa kufuata taratibu za ibada ili kuwatakasa kwa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa wengi waliokuwa katika lile kusanyiko walikuwa hawajajitakasa, iliwapasa Walawi wachinje wana-kondoo wengine wa Pasaka kwa ajili ya wale watu ambao hawakuwa safi, kwa kufuata taratibu za ibada ili kuwatakasa kwa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana kulikuwa na wengi katika kusanyiko ambao hawajajitakasa; kwa hiyo Walawi wakamchinjia Pasaka, kila mtu asiyekuwa safi, ili kuwatakasa kwa BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa vile wengi wa wale waliokusanyika hapo hawakuwa wamejitakasa, iliwabidi Walawi kuwachinjia wanakondoo wa Pasaka na kuwaweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani katika huo mkutano walikuwako wengi wasiojieua; kwa sababu hii Walawi wakawachinjia wote wasiotakata wana kondoo wa Pasaka, wawatakase kuwa wa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana kulikuwa na wengi katika kusanyiko ambao hawajajitakasa; kwa hiyo Walawi wakamchinjia pasaka, kila mtu asiyekuwa safi, ili kuwatakasa kwa BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa vile ambavyo wengi wa wale waliokusanyika pale hawakukuwa wamejitakasa. Walawi walipaswa kuwachinjia wana-kondoo wa Pasaka na kuwatakasa kwa ajili ya Yawe.