2 Chronicles 30:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Hezekia aliwasifu na kuwatia moyo makuhani kwa kuwa waliendesha ibada kwa ujuzi mwingi. Baada ya kumaliza siku saba wakati ambao watu walikula, wakatoa sadaka za amani na kumtukuza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hezekia akazungumza akiwatia moyo Walawi wote, ambao walionesha ustadi katika kumtumikia Mwenyezi Mungu. Hivyo watu wakala chakula cha sikukuu kwa siku saba, wakitoa sadaka za amani na kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hezekia akawafurahisha mioyo Walawi wote waliokuwa wastadi wa kumtumikia Bwana. Basi muda wa siku saba wakala sikukuu, wakitoa dhabihu za sadaka za amani, na kumtolea shukrani Bwana, Mungu wa baba zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Hezekia aliwasifu na kuwatia moyo makuhani kwa kuwa waliendesha ibada kwa ujuzi mwingi. Baada ya kumaliza siku saba wakati ambao watu walikula, wakatoa sadaka za amani na kumtukuza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hezekia akazungumza akiwatia moyo Walawi wote, ambao walionyesha ustadi katika kumtumikia BWANA. Hivyo watu wakala chakula cha sikukuu kwa siku saba, wakitoa dhabihu za amani na kumshukuru BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hezekia akazungumza akiwatia moyo Walawi wote, ambao walionyesha ustadi katika kumtumikia bwana. Hivyo watu wakala chakula cha sikukuu kwa siku saba, wakitoa sadaka za amani na kumshukuru bwana, Mungu wa baba zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hezekia akawafurahisha mioyo Walawi wote waliokuwa mastadi wa kumtumikia BWANA. Basi muda wa siku saba wakala sikukuu, wakitoa dhabihu za sadaka za amani, na kumtolea shukrani BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Hezekia aliwasifu na kuwatia moyo makuhani kwa kuwa waliendesha ibada kwa ujuzi mwingi. Baada ya kumaliza siku saba wakati ambao watu walikula, wakatoa sadaka za amani na kumtukuza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Hizikia akawaambia Walawi wote waliokuwa wenye akili njema katika kazi ya Bwana maneno yaliyoingia mioyoni mwao, wakaila sikukuu hii ya ushahidi siku saba, wakitoa vipaji vya tambiko vya shukrani, wamshukuru Bwana Mungu wa baba zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hezekia akawafurahisha mioyo Walawi wote waliokuwa wastadi wa kumtumikia BWANA. Basi muda wa siku saba wakala sikukuu, wakitoa dhabihu za sadaka za amani, na kumtolea shukrani BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Hezekia aliwasifu na kuwatia moyo makuhani kwa sababu waliendesha ibada kwa ujuzi mwingi. Nyuma ya kumaliza siku saba ambamo watu walikula, wakatoa sadaka za amani na kumutukuza Yawe, Mungu wa babu zao,