2 Chronicles 30:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Hezekia wa Yuda aliwapa watu waliokusanyika jumla ya mafahali 1,000 na kondoo 7,000. Hali kadhalika, wakuu wakawapa mafahali 1,000 na kondoo 10,000. Idadi kubwa ya makuhani walijitakasa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hezekia, mfalme wa Yuda akatoa mafahali elfu moja, kondoo na mbuzi elfu saba kwa ajili ya kusanyiko, nao maafisa wakatoa mafahali elfu moja, pamoja na kondoo na mbuzi elfu kumi. Idadi kubwa ya makuhani wakajiweka wakfu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Hezekia, mfalme wa Yuda, aliwatolea kusanyiko matoleo ya ng'ombe elfu, na kondoo elfu saba; na wakuu wakawatolea kusanyiko ng'ombe elfu, na kondoo elfu kumi; tena wakajitakasa makuhani wengi sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Hezekia wa Yuda aliwapa watu waliokusanyika jumla ya mafahali 1,000 na kondoo 7,000. Hali kadhalika, wakuu wakawapa mafahali 1,000 na kondoo 10,000. Idadi kubwa ya makuhani walijitakasa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hezekia, mfalme wa Yuda akatoa mafahali 1,000, kondoo na mbuzi 7,000 kwa ajili ya kusanyiko, nao maafisa wakatoa mafahali 1,000 pamoja na kondoo na mbuzi 10,000. Idadi kubwa ya makuhani wakajiweka wakfu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hezekia, mfalme wa Yuda akatoa mafahali 1,000, kondoo na mbuzi 7,000 kwa ajili ya kusanyiko, nao maafisa wakatoa mafahali 1,000 pamoja na kondoo na mbuzi 10,000. Idadi kubwa ya makuhani wakajiweka wakfu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana Hezekia, mfalme wa Yuda, aliwatolea kusanyiko matoleo ya ng'ombe elfu moja, na kondoo elfu saba; na wakuu wakawatolea kusanyiko ng'ombe elfu moja, na kondoo elfu kumi; tena wakajitakasa makuhani wengi sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Hezekia wa Yuda aliwapa watu waliokusanyika jumla ya mafahali 1,000 na kondoo 7,000. Hali kadhalika, wakuu wakawapa mafahali 1,000 na kondoo 10,000. Idadi kubwa ya makuhani walijitakasa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Hizikia, mfalme wa Wayuda, aliutolea huo mkutano madume ya ng'ombe 1000 na mbuzi na kondoo 7000, nao wakuu waliutolea mkutano madume ya ng'ombe 1000 na mbuzi na kondoo 7000; nao watambikaji walijieua wengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana Hezekia, mfalme wa Yuda, aliwatolea kusanyiko matoleo ya ng’ombe elfu, na kondoo elfu saba; na wakuu wakawatolea kusanyiko ng’ombe elfu, na kondoo elfu kumi; tena wakajitakasa makuhani wengi sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Hezekia wa Yuda akawapa watu waliokusanyika jumla ya ngombe dume elfu moja na kondoo elfu saba. Vilevile, wakubwa wakawapa ngombe dume elfu moja na kondoo elfu kumi. Hesabu kubwa ya makuhani wakajitakasa.