2 Chronicles 30:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
badala ya mwezi wa kwanza kama ilivyokuwa kawaida, kwa sababu idadi ya makuhani waliokuwa wamekwisha kujiweka wakfu ilikuwa ndogo, nao watu walikuwa bado hawajakusanyika Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu makuhani hawakuwa wamejitakasa ya kutosha na watu wakawa hawajakusanyika huko Yerusalemu, hawakuwa wameweza kuadhimisha Pasaka kwa wakati wake wa kawaida.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hawakuweza kuifanya wakati ule, kwa kuwa makuhani walikuwa hawajajitakasa wa kutosha, wala watu hawajakusanyika huko Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
badala ya mwezi wa kwanza kama ilivyokuwa kawaida, kwa sababu idadi ya makuhani waliokuwa wamekwisha kujiweka wakfu ilikuwa ndogo, nao watu walikuwa bado hawajakusanyika Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu makuhani hawakuwa wamejitakasa idadi ya kutosha na watu wakawa hawajakusanyika huko Yerusalemu, hawakuwa wameweza kuadhimisha Pasaka kwa wakati wake wa kawaida.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu makuhani hawakuwa wamejitakasa idadi ya kutosha na watu wakawa hawajakusanyika huko Yerusalemu, hawakuwa wameweza kuadhimisha Pasaka kwa wakati wake wa kawaida.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hawakuweza kuifanya wakati ule, kwa kuwa makuhani wa kutosha walikuwa hawajajitakasa, wala watu hawajakusanyika huko Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
badala ya mwezi wa kwanza kama ilivyokuwa kawaida, kwa sababu idadi ya makuhani waliokuwa wamekwisha kujiweka wakfu ilikuwa ndogo, nao watu walikuwa bado hawajakusanyika Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani hawakuweza kuila siku zile, kwa kuwa watambikaji wa kutosha hawajajieua, nao watu hawakukusanyika Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hawakuweza kuifanya wakati ule, kwa kuwa makuhani walikuwa hawajajitakasa wa kutosha, wala watu hawajakusanyika huko Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
pahali pa mwezi wa kwanza kama vile ilivyokuwa kawaida, kwa sababu hesabu ya makuhani waliokuwa wamekwisha kujitakasa ilikuwa ndogo, nao watu walikuwa bado hawajakusanyika Yerusalema.