2 Chronicles 30:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Matarishi, kwa amri yake mfalme na maofisa wake, walipeleka barua kote nchini Israeli na Yuda. Barua hizo zilikuwa na ujumbe ufuatao: “Enyi watu wa Israeli mlionusurika baada ya mashambulizi ya wafalme wa Ashuru. Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Israeli, ili naye apate kuwarudieni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa amri ya mfalme, matarishi wakazunguka Israeli na Yuda kote wakiwa na barua kutoka kwa mfalme na kutoka kwa maafisa wake, zilizoandikwa: “Watu wa Israeli, mrudieni Mwenyezi Mungu, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Israeli, ili naye awarudie ninyi mliosalia, mlionusurika kutoka mikononi mwa wafalme wa Ashuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaenda matarishi wenye nyaraka za mfalme na wakuu wake, kati ya Israeli yote na Yuda, na kwa amri ya mfalme, kusema, Enyi wana wa Israeli, mrudieni Bwana, Mungu wa Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, apate kuwarudia waliosalia wenu waliookoka mikononi mwa wafalme wa Ashuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Matarishi, kwa amri yake mfalme na maofisa wake, walipeleka barua kote nchini Israeli na Yuda. Barua hizo zilikuwa na ujumbe ufuatao: “Enyi watu wa Israeli mlionusurika baada ya mashambulizi ya wafalme wa Ashuru. Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Israeli, ili naye apate kuwarudieni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa amri ya mfalme, matarishi wakapita katika Israeli na Yuda kote wakiwa na barua kutoka kwa mfalme na kutoka kwa maafisa wake zikisema: “Watu wa Israeli, mrudieni BWANA, Mungu wa Abrahamu, Isaki na Israeli, ili naye awarudie ninyi mliosalia, mlionusurika kutoka mikononi mwa wafalme wa Ashuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa amri ya mfalme, matarishi wakapita katika Israeli na Yuda kote wakiwa na barua kutoka kwa mfalme na kutoka kwa maafisa wake zikisema: “Watu wa Israeli, mrudieni bwana, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Israeli, ili naye awarudie ninyi mliosalia, mlionusurika kutoka mikononi mwa wafalme wa Ashuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Matarishi, kwa amri ya mfalme na maofisa wake wakapeleka nyaraka katika Israeli na Yuda yote, kusema, Enyi wana wa Israeli, mrudieni BWANA, Mungu wa Abrahamu, na Isaka, na Israeli, apate kuwarudia ninyi mlionusurika na kuokoka toka mikononi mwa Wafalme wa Ashuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Matarishi, kwa amri yake mfalme na maofisa wake, walipeleka barua kote nchini Israeli na Yuda. Barua hizo zilikuwa na ujumbe ufuatao: “Enyi watu wa Israeli mlionusurika baada ya mashambulizi ya wafalme wa Ashuru. Mrudieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Israeli, ili naye apate kuwarudieni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wajumbe wapigao mbio wakaenda na barua, walizopewa na mfalme na wakuu wake, katika nchi zote za Waisiraeli na za Wayuda, wakasema, kama walivyoagizwa na mfalme: Wana wa Isiraeli rudini kwake Bwana, Mungu wa Aburahamu na wa Isaka na wa Isiraeli! Ndipo, atakaporudi kwao waliosalia kwenu kwa kupona mikononi mwa wafalme wa Asuri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaenda matarishi wenye nyaraka za mfalme na wakuu wake, kati ya Israeli yote na Yuda, na kwa amri ya mfalme, kusema, Enyi wana wa Israeli, mrudieni BWANA, Mungu wa Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, apate kuwarudia waliosalia wenu waliookoka mikononi mwa wafalme wa Ashuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo wajumbe wakapita katika inchi yote ya Israeli na ya Yuda kwa kupeleka barua zile kufuatana na amri ya mufalme na wakubwa wake. Barua hizo zilikuwa na ujumbe huu: “Enyi watu wa Israeli muliobaki nyuma ya mashambulizi ya wafalme wa Asuria. Mumurudilie Yawe, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Israeli, kusudi naye apate kuwarudilia.