2 Chronicles 31:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya sherehe kumalizika, watu wote wa Israeli walikwenda katika kila mji wa Yuda, wakavunjavunja nguzo za mawe na kuzikatakata sanamu za Ashera, mungu wa kike, na pia wakaziharibu madhabahu na mahali pa kuabudia miungu mingine. Walifanya vivyo hivyo kote katika Yuda, Benyamini, Efraimu na Manase, mpaka walipokwisha kuharibu vyote. Kisha wakarudi mjini mwao, kila mtu kwenye milki yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya mambo haya yote kumalizika, Waisraeli ambao walikuwa huko wakaenda kwenye miji ya Yuda, wakayavunja yale mawe ya kuabudia na kuzikatakata zile nguzo za Ashera. Wakabomoa mahali pa juu pa kuabudia pamoja na madhabahu zake kila mahali katika Yuda na Benyamini, na katika Efraimu na Manase. Baada ya kuviharibu hivi vyote, Waisraeli wakarudi miji yao wenyewe na kwenye milki zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi hayo yote yalipokwisha, wakatoka Israeli wote waliokuwako waende miji ya Yuda, wakazivunja-vunja nguzo, wakayakata-kata maashera, wakabomoa mahali pa juu na madhabahu katika Yuda yote na Benyamini, katika Efraimu pia na Manase, hata walipokwisha kuviharibu vyote. Ndipo wana wa Israeli wote wakarudi, kila mtu kwa milki yake, mijini kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya sherehe kumalizika, watu wote wa Israeli walikwenda katika kila mji wa Yuda, wakavunjavunja nguzo za mawe na kuzikatakata sanamu za Ashera, mungu wa kike, na pia wakaziharibu madhabahu na mahali pa kuabudia miungu mingine. Walifanya vivyo hivyo kote katika Yuda, Benyamini, Efraimu na Manase, mpaka walipokwisha kuharibu vyote. Kisha wakarudi mjini mwao, kila mtu kwenye milki yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya mambo haya yote kumalizika, Waisraeli ambao walikuwako huko wakaenda kwenye miji ya Yuda, wakayavunja yale mawe ya kuabudia na kuzikatakata zile nguzo za Ashera. Wakabomoa mahali pa juu pa kuabudia miungu pamoja na madhabahu zake kila mahali katika Yuda na Benyamini na katika Efraimu na Manase. Baada ya kuviharibu hivi vyote, Waisraeli wakarudi katika miji yao wenyewe na kwenye milki zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya mambo haya yote kumalizika, Waisraeli ambao walikuwako huko wakaenda kwenye miji ya Yuda, wakayavunja yale mawe ya kuabudia na kuzikatakata zile nguzo za Ashera. Wakabomoa mahali pa juu pa kuabudia miungu pamoja na madhabahu zake kila mahali katika Yuda na Benyamini na katika Efraimu na Manase. Baada ya kuviharibu hivi vyote, Waisraeli wakarudi katika miji yao wenyewe na kwenye milki zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi hayo yote yalipokwisha, Israeli wote waliokuwako wakatoka waende miji ya Yuda, wakazivunjavunja nguzo, wakayakatakata Maashera, wakabomoa mahali pa juu na madhabahu katika Yuda yote na Benyamini, katika Efraimu pia na Manase, hadi walipoviharibu vyote. Ndipo wana wa Israeli wote wakarudi, kila mtu kwa milki yake, mijini kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya sherehe kumalizika, watu wote wa Israeli walikwenda katika kila mji wa Yuda, wakavunjavunja nguzo za mawe na kuzikatakata sanamu za Ashera, mungu wa kike, na pia wakaziharibu madhabahu na mahali pa kuabudia miungu mingine. Walifanya vivyo hivyo kote katika Yuda, Benyamini, Efraimu na Manase, mpaka walipokwisha kuharibu vyote. Kisha wakarudi mjini mwao, kila mtu kwenye milki yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipokwisha kuyamaliza hayo yote, Waisiraeli wote waliokuwako wakatoka kwenda zao katika miji ya Yuda, wakazivunja nguzo za kutambikia, wakaikatakata nayo miti ya Ashera, wakavibomoa vijumba vya kutambikia vilimani pamoja na meza zao za kutambikia katika nchi zote za Yuda na za Benyamini na za Efuraimu na za Manase, mpaka wakavitowesha kabisa hivyo vyote, kisha wana wote wa Isiraeli wakarudi kila mtu mahali palipokuwamali yake katika miji yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi hayo yote yalipokwisha, wakatoka Israeli wote waliokuwako waende miji ya Yuda, wakazivunja-vunja nguzo, wakayakata-kata maashera, wakabomoa mahali pa juu na madhabahu katika Yuda yote na Benyamini, katika Efraimu pia na Manase, hata walipokwisha kuviharibu vyote. Ndipo wana wa Israeli wote wakarudi, kila mtu kwa milki yake, mijini kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya sherehe kumalizika, watu wote wa Israeli wakakwenda katika kila muji wa Yuda, wakavunjavunja nguzo za mawe na kukatakata sanamu za Ashera, mungu wa kike, na vilevile wakaharibu mazabahu na pahali pa kuabudia miungu mingine. Wakafanya vile katika inchi yote ya Yuda, Benjamina, Efuraimu na Manase, mpaka walipokwisha kuvimaliza vyote. Kisha Waisraeli wakarudi kwao, kila mutu kwenye urizi wake.