2 Chronicles 31:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Azaria, kuhani mkuu aliyekuwa wa uzao wa Sadoki akamjibu, “Tangu watu waanze kuleta matoleo yao hekaluni, tumekuwa na vyakula vya kutosha na hata tunayo akiba kubwa. Mwenyezi-Mungu amewabariki watu wake, ndiyo maana tumepata vitu hivi vyote.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
naye Azaria aliyekuwa kuhani mkuu, kutoka jamaa ya Sadoki, akajibu, “Tangu watu walipoanza kuleta sadaka zao katika Hekalu la Mwenyezi Mungu tumekuwa na chakula cha kutosha na vingi vya kuweka akiba kwa sababu Mwenyezi Mungu amewabariki watu wake, hivyo tumekuwa na kiasi kingi kilichobaki.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Azaria kuhani mkuu, wa nyumba ya Sadoki, akamjibu, akasema, Tangu watu walipoanza kuleta matoleo nyumbani kwa Bwana, tumekula na kushiba, na kusaza tele; kwa kuwa Bwana amewabariki watu wake; na kilichosalia ndiyo akiba hii kubwa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Azaria, kuhani mkuu aliyekuwa wa uzao wa Sadoki akamjibu, “Tangu watu waanze kuleta matoleo yao hekaluni, tumekuwa na vyakula vya kutosha na hata tunayo akiba kubwa. Mwenyezi-Mungu amewabariki watu wake, ndiyo maana tumepata vitu hivi vyote.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
naye Azaria aliyekuwa Kuhani Mkuu, kutoka jamaa ya Sadoki, akajibu, “Tangu watu walipoanza kuleta sadaka zao katika Hekalu la BWANA tumekuwa na chakula cha kutosha na vingi vya kuweka akiba kwa sababu BWANA amewabariki watu wake, hivyo tumekuwa na kiasi kingi kilichobaki.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
naye Azaria aliyekuwa kuhani mkuu, kutoka jamaa ya Sadoki, akajibu, “Tangu watu walipoanza kuleta sadaka zao katika Hekalu la bwana tumekuwa na chakula cha kutosha na vingi vya kuweka akiba kwa sababu bwana amewabariki watu wake, hivyo tumekuwa na kiasi kingi kilichobaki.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Azaria kuhani mkuu, wa nyumba ya Sadoki, akamjibu, akasema, Tangu watu walipoanza kuleta matoleo nyumbani kwa BWANA, tumekula na kushiba, na kusaza tele; kwa kuwa BWANA amewabariki watu wake; na kilichosalia ndiyo akiba hii kubwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Azaria, kuhani mkuu aliyekuwa wa uzao wa Sadoki akamjibu, “Tangu watu waanze kuleta matoleo yao hekaluni, tumekuwa na vyakula vya kutosha na hata tunayo akiba kubwa. Mwenyezi-Mungu amewabariki watu wake, ndiyo maana tumepata vitu hivi vyote.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Azaria aliyekuwa mtambikaji mkuu wa mlango wa Sadoki akamjibu, akamwambia: Tangu hapo, walipoanza kuyaleta haya matoleo Nyumbani mwa Bwana, tumekula na kushiba, nayo haya mengi ndiyo yaliyosalia, kwani Bwana amewabariki walio ukoo wake, kwa hiyo vimesalia hivyo vipaji vingi mno.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Azaria kuhani mkuu, wa nyumba ya Sadoki, akamjibu, akasema, Tangu watu walipoanza kuleta matoleo nyumbani kwa BWANA, tumekula na kushiba, na kusaza tele; kwa kuwa BWANA amewabariki watu wake; na kilichosalia ndiyo akiba hii kubwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Azaria, Kuhani Mukubwa aliyekuwa wa uzao wa Sadoki akamujibu: “Tangu wakati watu walipoanza kuleta matoleo yao katika hekalu, tumekuwa na vyakula vya kutosha na hata tuna akiba kubwa. Yawe amewabariki watu wake, ndiyo maana tumepata vitu hivi vyote.”