2 Chronicles 31:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na humo wakaweka matoleo, zaka na vyote vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu. Wakamweka Konania, Mlawi, awe ofisa mkuu mtunzaji wa vitu hivyo, na Shimei nduguye, awe msaidizi wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha kwa uaminifu wakaleta sadaka zao, mafungu yao ya kumi na vitu vilivyowekwa wakfu. Konania Mlawi, ndiye alikuwa msimamizi wa vitu hivi na Shimei ndugu yake ndiye alikuwa msaidizi wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakayaingiza matoleo na zaka na vitu vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu; na juu yake Konania Mlawi alikuwa mkuu, na wa pili ni Shimei nduguye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na humo wakaweka matoleo, zaka na vyote vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu. Wakamweka Konania, Mlawi, awe ofisa mkuu mtunzaji wa vitu hivyo, na Shimei nduguye, awe msaidizi wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha kwa uaminifu wakaleta sadaka zao, mafungu yao ya kumi na vitu vilivyowekwa wakfu. Konania Mlawi, ndiye aliyekuwa msimamizi wa vitu hivi na Shimei ndugu yake ndiye aliyekuwa msaidizi wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha kwa uaminifu wakaleta sadaka zao, mafungu yao ya kumi na vitu vilivyowekwa wakfu. Konania Mlawi, ndiye alikuwa msimamizi wa vitu hivi na Shimei ndugu yake ndiye alikuwa msaidizi wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakayaingiza matoleo na zaka na vitu vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu; Konania, Mlawi aliwekwa kuwa mkuu na Shimei nduguye akawa masaidizi wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na humo wakaweka matoleo, zaka na vyote vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu. Wakamweka Konania, Mlawi, awe ofisa mkuu mtunzaji wa vitu hivyo, na Shimei nduguye, awe msaidizi wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wao kwa kuwa welekevu wakaingiza humo yale matoleo na mafungu ya kumi na vipaji vitakatifu vyote pia, Mlawi Konania akawekwa kuyaangalia, naye ndugu yake Simei akawa wa pili.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakayaingiza matoleo na zaka na vitu vilivyowekwa wakfu, kwa uaminifu; na juu yake Konania Mlawi alikuwa mkuu, na wa pili ni Shimei nduguye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na mule ndani wakaweka matoleo, sehemu moja za kumi na vyote vilivyotakaswa kwa uaminifu. Wakamuweka Konania, Mulawi, kuwa musimamizi mukubwa muchungaji wa vitu hivyo, na ndugu yake, Simea kuwa musaidizi wake.