2 Chronicles 31:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena, bila kujali koo walimoandikishwa, waliwapa sehemu wale watoto wa kiume waliokuwa wametimiza umri wa miaka mitatu na zaidi, na ambao waliingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kila siku kutekeleza wajibu wao. Kila mmoja wao alipata sehemu yake kulingana na huduma aliyotoa kwa zamu yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hao wakawagawia wanaume wenye umri wa miaka mitatu au zaidi ambao majina yao yalikuwa kwenye orodha ya vizazi, wale wote ambao wangeingia katika Hekalu la Mwenyezi Mungu ili kufanya kazi zao mbalimbali za kila siku kulingana na wajibu katika mgawanyo wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
zaidi ya wale waliohesabiwa kwa nasaba ya wanaume, wenye miaka mitatu na zaidi, kila mmoja aliyeingia nyumbani mwa Bwana, kama ilivyopasa kazi ya kila siku, kwa huduma zao katika malinzi yao, kwa kadiri ya zamu zao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena, bila kujali koo walimoandikishwa, waliwapa sehemu wale watoto wa kiume waliokuwa wametimiza umri wa miaka mitatu na zaidi, na ambao waliingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kila siku kutekeleza wajibu wao. Kila mmoja wao alipata sehemu yake kulingana na huduma aliyotoa kwa zamu yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hao wakawagawia wanaume wenye umri wa miaka mitatu au zaidi ambao majina yao yalikuwa kwenye orodha ya vizazi, wale wote ambao wangeingia katika Hekalu la BWANA ili kufanya kazi zao mbalimbali za kila siku kulingana na wajibu katika mgawanyo wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hao wakawagawia wanaume wenye umri wa miaka mitatu au zaidi ambao majina yao yalikuwa kwenye orodha ya vizazi, wale wote ambao wangeingia katika Hekalu la bwana ili kufanya kazi zao mbalimbali za kila siku kulingana na wajibu katika mgawanyo wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
zaidi ya wale waliohesabiwa kwa nasaba ya wanaume, wenye miaka mitatu na zaidi, kila mmoja aliyeingia nyumbani mwa BWANA, kama ilivyopasa kazi ya kila siku, kwa huduma zao katika sehemu yao, kwa kadiri ya zamu zao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena, bila kujali koo walimoandikishwa, waliwapa sehemu wale watoto wa kiume waliokuwa wametimiza umri wa miaka mitatu na zaidi, na ambao waliingia katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu kila siku kutekeleza wajibu wao. Kila mmoja wao alipata sehemu yake kulingana na huduma aliyotoa kwa zamu yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kuliko wale wanawaume walioandikwa katika kitabu chao walio wa miaka mitatu na zaidi; nao hawa ndio wote waingiao Nyumbani mwa Bwana kwa mambo ya kila siku moja kufanya kazi za utumishi wao ziwapasazo kuziangalia kwa zamu zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
zaidi ya wale waliohesabiwa kwa nasaba ya wanaume, wenye miaka mitatu na zaidi, kila mmoja aliyeingia nyumbani mwa BWANA, kama ilivyopasa kazi ya kila siku, kwa huduma zao katika malinzi yao, kwa kadiri ya zamu zao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena, bila kujali ukoo walimoandikishwa, waliwapa sehemu wale watoto wa kiume waliokuwa wametimiza umri wa miaka mitatu na zaidi, na ambao waliingia katika nyumba ya Yawe kila siku kwa kutimiza kazi zao. Kila mumoja wao alipata sehemu yake kulingana na kazi aliyofanya kwa zamu yake.