2 Chronicles 31:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Vilevile, miongoni mwa wazawa wa Aroni, makuhani waliokuwa wanakaa katika mashamba waliyomiliki kwa pamoja nje ya miji yao, mlikuwa watu maalumu kwenye miji hiyo ambao waliwagawia sehemu zao za vyakula. Waliwapa sehemu kila mwanamume katika jamaa za makuhani, na kila mmoja aliyekuwa ameandikishwa kati ya Walawi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuhusu makuhani, wazao wa Haruni walioishi kwenye mashamba yaliyozunguka miji yao au katika miji mingine yoyote, watu walitajwa majina ili kumgawia kila mwanaume miongoni mwao na kwa wote waliokuwa katika orodha ya vizazi vya Walawi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
tena kwa ajili ya wana wa Haruni makuhani, waliokuwamo mashambani mwa malisho ya miji yao, mji kwa mji, kulikuwa na watu waliotajwa majina yao, ili kuwagawia sehemu wanaume wote miongoni mwa makuhani, na wote waliohesabiwa kwa nasaba miongoni mwa Walawi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Vilevile, miongoni mwa wazawa wa Aroni, makuhani waliokuwa wanakaa katika mashamba waliyomiliki kwa pamoja nje ya miji yao, mlikuwa watu maalumu kwenye miji hiyo ambao waliwagawia sehemu zao za vyakula. Waliwapa sehemu kila mwanamume katika jamaa za makuhani, na kila mmoja aliyekuwa ameandikishwa kati ya Walawi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuhusu makuhani, wazao wa Aroni walioishi kwenye mashamba yaliyozunguka miji yao au katika miji mingine yo yote, watu walitajwa majina ili kumgawia kila mwanaume miongoni mwao na kwa wote ambao walikuwa katika orodha ya vizazi vya Walawi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuhusu makuhani, wazao wa Haruni walioishi kwenye mashamba yaliyozunguka miji yao au katika miji mingine yoyote, watu walitajwa majina ili kumgawia kila mwanaume miongoni mwao na kwa wote waliokuwa katika orodha ya vizazi vya Walawi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
tena kwa ajili ya wana wa Haruni makuhani, waliokuwamo mashambani mwa malisho ya miji yao, mji kwa mji, kulikuwa na watu waliotajwa majina yao, ili kuwagawia sehemu wanaume wote miongoni mwa makuhani, na wote waliohesabiwa kwa nasaba miongoni mwa Walawi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Vilevile, miongoni mwa wazawa wa Aroni, makuhani waliokuwa wanakaa katika mashamba waliyomiliki kwa pamoja nje ya miji yao, mlikuwa watu maalumu kwenye miji hiyo ambao waliwagawia sehemu zao za vyakula. Waliwapa sehemu kila mwanamume katika jamaa za makuhani, na kila mmoja aliyekuwa ameandikishwa kati ya Walawi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wana wa Haroni waliokuwa watambikaji mashambani kwenye mitaa ya miji yao wakapata watu katika kila mji mmoja walioandikwa majina yao, wawagawie yawapasayo, kila mume mmoja fungu lake miongoni mwa watambikaji, namo mwa Walawi wote walioandikwa katika kitabu cha udugu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
tena kwa ajili ya wana wa Haruni makuhani, waliokuwamo mashambani mwa malisho ya miji yao, mji kwa mji, kulikuwa na watu waliotajwa majina yao, ili kuwagawia sehemu wanaume wote miongoni mwa makuhani, na wote waliohesabiwa kwa nasaba miongoni mwa Walawi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Vilevile, kati ya wazao wa Haruni, makuhani waliokuwa wanakaa katika mashamba waliyorizi kwa pamoja inje ya miji yao, kulikuwa watu waliochaguliwa kwenye miji hiyo ambao waliwagawanyia sehemu zao za vyakula. Waliwapa sehemu kila mwanaume katika jamaa za makuhani, na kila mumoja aliyekuwa ameandikishwa kati ya Walawi.