2 Chronicles 31:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme Hezekia aliwapanga tena makuhani na Walawi katika makundi, akampa kila mmoja wao wajibu maalumu, kuhudumu katika sehemu mbalimbali za hekalu la Mwenyezi-Mungu. Wajibu huo ni pamoja na utoaji wa sadaka za kuteketeza na za amani, kushukuru na kusifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hezekia akawapanga makuhani na Walawi katika migawanyo, kila mgawanyo kulingana na wajibu wao, kama ni makuhani au Walawi, ili kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, kuhudumu, kushukuru na kuimba sifa katika malango ya makao ya Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hezekia akaziweka zamu za makuhani na Walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadiri ya huduma yake, makuhani na Walawi pia, kwa sadaka za kuteketezwa na kwa sadaka za amani, kutumika, na kushukuru, na kusifu, malangoni mwa matuo ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme Hezekia aliwapanga tena makuhani na Walawi katika makundi, akampa kila mmoja wao wajibu maalumu, kuhudumu katika sehemu mbalimbali za hekalu la Mwenyezi-Mungu. Wajibu huo ni pamoja na utoaji wa sadaka za kuteketeza na za amani, kushukuru na kusifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hezekia akawapanga makuhani na Walawi katika migawanyo, kila mgawanyo kulingana na wajibu wao, kama ni makuhani au Walawi, ili kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, kuhudumu, kushukuru na kuimba sifa katika malango ya makao ya BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hezekia akawapanga makuhani na Walawi katika migawanyo, kila mgawanyo kulingana na wajibu wao, kama ni makuhani au Walawi, ili kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, kuhudumu, kushukuru na kuimba sifa katika malango ya makao ya bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hezekia akaziweka zamu za makuhani na Walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadiri ya huduma yake, makuhani na Walawi pia, kwa sadaka za kuteketezwa na kwa sadaka za amani, kutumika, na kushukuru, na kusifu, malangoni mwa kambi ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme Hezekia aliwapanga tena makuhani na Walawi katika makundi, akampa kila mmoja wao wajibu maalumu, kuhudumu katika sehemu mbalimbali za hekalu la Mwenyezi-Mungu. Wajibu huo ni pamoja na utoaji wa sadaka za kuteketeza na za amani, kushukuru na kusifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Hizikia akaweka kazi za zamu za watambikaji na za Walawi zizipasazo zamu zao, kila mtu akawa na kazi yake ya utumishi wake, watambikaji na Walawi: kuteketeza ng'ombe za tambiko na kutengeneza ng'ombe za tambiko za shukrani na kutumikia malangoni kwa matuo yake Bwana na kumshukuru na kumshangilia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hezekia akaziweka zamu za makuhani na Walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadiri ya huduma yake, makuhani na Walawi pia, kwa sadaka za kuteketezwa na kwa sadaka za amani, kutumika, na kushukuru, na kusifu, malangoni mwa matuo ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme Hezekia akawapanga tena makuhani na Walawi katika makundi, akamupa kila mumoja wao kazi kufuatana na utumishi wake katika sehemu mbalimbali za hekalu la Yawe. Kazi ile ni pamoja na utoaji wa sadaka za kuteketeza kwa moto na za amani, za shukrani na za kusifu.