2 Chronicles 31:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mara tu amri hii ilipotolewa, watu wa Israeli walitoa kwa wingi, malimbuko ya nafaka, divai, mafuta, asali na mazao mengine mbalimbali ya shambani, na pia zaka nyingi za kila kitu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mara tu baada ya kutolewa tangazo hilo, Waisraeli wakatoa kwa ukarimu malimbuko ya nafaka zao, divai mpya, mafuta na asali pamoja na vyote vilivyotoka mashambani. Wakaleta kiasi kikubwa cha fungu la kumi la kila kitu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mara ilipotangaa amri, wana wa Israeli wakatoa kwa wingi malimbuko ya nafaka, na divai, na mafuta, na asali, na mazao yote ya mashamba; na zaka za vitu vyote wakazileta nyingi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mara tu amri hii ilipotolewa, watu wa Israeli walitoa kwa wingi, malimbuko ya nafaka, divai, mafuta, asali na mazao mengine mbalimbali ya shambani, na pia zaka nyingi za kila kitu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mara tu baada ya kutolewa tangazo hilo, Waisraeli wakatoa kwa ukarimu malimbuko ya nafaka zao, divai mpya, mafuta na asali pamoja na vyote vilivyotoka mashambani. Wakaleta kiasi kikubwa cha fungu la kumi la kila kitu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mara tu baada ya kutolewa tangazo hilo, Waisraeli wakatoa kwa ukarimu malimbuko ya nafaka zao, divai mpya, mafuta na asali pamoja na vyote vilivyotoka mashambani. Wakaleta kiasi kikubwa cha fungu la kumi la kila kitu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mara amri ilipovavagaa, wana wa Israeli wakatoa kwa wingi malimbuko ya nafaka, divai, mafuta, asali, na mazao yote ya mashamba; na zaka za vitu vyote wakazileta kwa wingi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mara tu amri hii ilipotolewa, watu wa Israeli walitoa kwa wingi, malimbuko ya nafaka, divai, mafuta, asali na mazao mengine mbalimbali ya shambani, na pia zaka nyingi za kila kitu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Agizo hili lilipoenea, wana wa Isiraeli wengi wakaleta malimbuko ya ngano na ya mvinyo na ya mafuta na ya asali na ya mazao yote ya mashamba, wakayaleta nayo mafungu ya kumi ya mali zote, yakawa mengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mara ilipotangaa amri, wana wa Israeli wakatoa kwa wingi malimbuko ya nafaka, na divai, na mafuta, na asali, na mazao yote ya mashamba; na zaka za vitu vyote wakazileta nyingi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mara tu amri hii ilipotolewa, watu wa Israeli wakatoa kwa wingi, malimbuko ya ngano, divai, mafuta, asali na mazao mengine mbalimbali ya shamba, na vilevile sehemu moja ya kumi ya kila kitu.