2 Chronicles 31:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda, pia wakaleta zaka zao za ng'ombe na kondoo na vitu vingine, wakaviweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Waliviweka vitu hivyo katika mafungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda wakaleta pia fungu la kumi la makundi yao ya ng’ombe na makundi ya kondoo na mbuzi pia na fungu la kumi la vitu vitakatifu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, na kuvikusanya katika malundo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao wana wa Israeli na Yuda, waliokaa mijini mwa Yuda, wakaleta pia zaka za ng'ombe na kondoo, na zaka za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyowekewa Bwana, Mungu wao, wakaviweka chungu chungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda, pia wakaleta zaka zao za ng'ombe na kondoo na vitu vingine, wakaviweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Waliviweka vitu hivyo katika mafungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda wakaleta pia fungu la kumi la makundi yao ya ng'ombe na makundi ya kondoo na mbuzi pia na fungu la kumi la vitu vitakatifu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya BWANA Mungu wao na kuvikusanya katika malundo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda wakaleta pia fungu la kumi la makundi yao ya ng’ombe na makundi ya kondoo na mbuzi pia na fungu la kumi la vitu vitakatifu vilivyowekwa wakfu kwa ajili ya bwana Mwenyezi Mungu wao na kuvikusanya katika malundo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao wana wa Israeli na Yuda, waliokaa mijini mwa Yuda, wakaleta pia zaka za ng'ombe na kondoo, na zaka za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyowekewa BWANA, Mungu wao, wakaviweka katika mafungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda, pia wakaleta zaka zao za ng'ombe na kondoo na vitu vingine, wakaviweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Waliviweka vitu hivyo katika mafungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wana wa Isiraeli na wa Yuda waliokaa katika miji ya Yuda wakaleta nayo mafungu ya kumi ya ng'ombe na ya mbuzi na ya kondoo nayo mafungu ya kumi ya vipaji vitakatifu vilivyotolewa kuwa mali za Bwana Mungu wao, wakaviweka machungu machungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao wana wa Israeli na Yuda, waliokaa mijini mwa Yuda, wakaleta pia zaka za ng’ombe na kondoo, na zaka za vitu vilivyowekwa wakfu, alivyowekewa BWANA, Mungu wao, wakaviweka chungu chungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Israeli na Yuda walioishi katika miji ya Yuda, wakaleta vilevile sehemu moja ya kumi ya ngombe na kondoo na ya vitu vitakatifu vilivyotolewa kwa Yawe. Wakaviweka vitu hivyo katika mafungu.