2 Chronicles 32:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya mambo yote hayo ya uaminifu ya mfalme Hezekia, mfalme Senakeribu wa Ashuru aliivamia Yuda. Alikuja akapiga makambi kwenye miji yenye ngome akitumaini kwamba ataishinda iwe mali yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya yale yote aliyokuwa amefanya Hezekia kwa uaminifu mkubwa, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaja na kuvamia Yuda. Akaizingira miji yenye ngome, akikusudia kuiteka iwe yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa, baada ya mambo hayo, na uaminifu huo, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akaja, akaingia katika Yuda, akafanya marago juu ya miji yenye maboma, akadhania kwamba ataipata iwe yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya mambo yote hayo ya uaminifu ya mfalme Hezekia, mfalme Senakeribu wa Ashuru aliivamia Yuda. Alikuja akapiga makambi kwenye miji yenye ngome akitumaini kwamba ataishinda iwe mali yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya yale yote aliyokuwa amefanya Hezekia kwa uaminifu mkubwa, Senakeribu, mfalme wa Ashuru akaja na kuivamia Yuda. Akaizunguka kwa jeshi miji yenye ngome, akifikiri kuiteka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya yale yote aliyokuwa amefanya Hezekia kwa uaminifu mkubwa, Senakeribu mfalme wa Ashuru akaja na kuvamia Yuda. Akaizunguka miji yenye ngome kwa jeshi, akifikiri kuiteka iwe yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa, baada ya mambo hayo, na uaminifu huo, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akaja, akaingia katika Yuda, akapiga kambi juu ya miji yenye maboma, akadhania kwamba ataipata iwe yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya mambo yote hayo ya uaminifu ya mfalme Hezekia, mfalme Senakeribu wa Ashuru aliivamia Yuda. Alikuja akapiga makambi kwenye miji yenye ngome akitumaini kwamba ataishinda iwe mali yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo yalipokwisha kufanyika kwa welekevu, akaja Saniheribu, mfalme wa Asuri; akaingia katika nchi ya Yuda, akapiga makambi kwenye miji yenye maboma, akataka kujipenyeza humo, iwe yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa, baada ya mambo hayo, na uaminifu huo, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akaja, akaingia katika Yuda, akafanya marago juu ya miji yenye maboma, akadhania kwamba ataipata iwe yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya matendo hayo ya uaminifu ya mufalme Hezekia, mufalme Saniharibu wa Asuria akashambulia inchi ya Yuda. Akakuja kupiga makambi kwenye miji yenye kuta akitumaini kwamba ataishinda ikuwe mali yake.