2 Chronicles 32:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni mungu gani kati ya miungu ya mataifa hayo iliyoharibiwa kabisa na babu zangu aliyeweza kuwakomboa watu wake kutoka mikononi mwangu ndio nanyi muwe na tumaini ya kwamba Mungu wenu atawaokoeni mikononi mwangu?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni yupi miongoni mwa miungu yote ya mataifa haya ambayo baba zangu waliyaangamiza ameweza kuwaokoa watu wake mkononi mwangu? Inawezekanaje basi Mungu wenu kuwaokoa mkononi mwangu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ni yupi miongoni mwa miungu ya mataifa wale walioharibiwa kabisa na baba zangu, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, hata Mungu wenu aweze kuwaokoa ninyi na mkono wangu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni mungu gani kati ya miungu ya mataifa hayo iliyoharibiwa kabisa na babu zangu aliyeweza kuwakomboa watu wake kutoka mikononi mwangu ndio nanyi muwe na tumaini ya kwamba Mungu wenu atawaokoeni mikononi mwangu?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni yupi miongoni mwa miungu yote ya mataifa haya ambayo baba zangu waliyaangamiza, iliyoweza kuwaokoa watu wake mkononi mwangu? Ni vipi basi Mungu wenu atakavyoweza kuwaokoa kutoka katika mkono wangu?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni yupi miongoni mwa miungu yote ya mataifa haya ambayo baba zangu waliyaangamiza ameweza kuwaokoa watu wake mkononi mwangu? Inawezekanaje basi Mungu wenu kuwaokoa mkononi mwangu?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ni yupi miongoni mwa miungu ya mataifa wale walioharibiwa kabisa na baba zangu, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, ndipo Mungu wenu aweze kuwaokoa ninyi na mkono wangu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni mungu gani kati ya miungu ya mataifa hayo iliyoharibiwa kabisa na babu zangu aliyeweza kuwakomboa watu wake kutoka mikononi mwangu ndio nanyi muwe na tumaini ya kwamba Mungu wenu atawaokoeni mikononi mwangu?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika miungu yote ya haya mataifa, baba zangu waliyoyatia mwiko wa kuwapo, ulikuwa upi ulioweza kuwaponya watu wake mkononi mwangu? Naye Mungu wenu atawezaje kuwaponya mkononi mwangu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ni yupi miongoni mwa miungu ya mataifa wale walioharibiwa kabisa na baba zangu, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, hata Mungu wenu aweze kuwaokoa ninyi na mkono wangu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni mungu gani kati ya miungu ya mataifa yale yaliyoharibiwa kabisa na babu zangu aliyeweza kuwakomboa watu wake kutoka katika mikono yangu ndiyo nanyi mukuwe na tumaini kwamba Mungu wenu atawaokoa toka mikono yangu?