2 Chronicles 32:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msidanganywe na Hezekia wala msishawishike kwa hayo. Msimwamini mtu huyu, kwa maana hapajatokea mungu wa taifa au mfalme yeyote aliyefaulu kuwakomboa watu wake kutoka mikononi mwa mfalme wa Ashuru, sembuse huyu Mungu wenu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sasa basi, msikubali Hezekia awadanganye na kuwapotosha namna hii. Msimwamini, kwa kuwa hakuna mungu wa taifa lolote wala wa ufalme wowote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka mkononi mwangu au mkononi mwa baba zangu. Sembuse huyo mungu wenu atawaokoaje kutoka mkononi mwangu!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi sasa asiwadanganye Hezekia, wala asiwashawishi kwa hayo, wala msimwamini; kwa kuwa hapana mungu wa taifa lo lote, wala wa ufalme wo wote, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, au na mkono wa baba zangu; sembuse Mungu wenu atawaokoaje ninyi na mkono wangu?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msidanganywe na Hezekia wala msishawishike kwa hayo. Msimwamini mtu huyu, kwa maana hapajatokea mungu wa taifa au mfalme yeyote aliyefaulu kuwakomboa watu wake kutoka mikononi mwa mfalme wa Ashuru, sembuse huyu Mungu wenu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sasa basi, msikubali Hezekia awadanganye nakuwapotosha namna hii. Msimwamini kwa kuwa hakuna mungu wa taifa lo lote wala wa ufalme wo wote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka mkononi mwangu au mkononi mwa baba zangu. Sembuse huyo Mungu wenu atawaokoaje kutoka mkononi mwangu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sasa basi, msikubali Hezekia awadanganye na kuwapotosha namna hii. Msimwamini, kwa kuwa hakuna mungu wa taifa lolote wala wa ufalme wowote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka mkononi mwangu au mkononi mwa baba zangu. Sembuse huyo mungu wenu atawaokoaje kutoka mkononi mwangu!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi sasa asiwadanganye Hezekia, wala asiwashawishi kwa hayo, wala msimwamini; kwa kuwa hapana mungu wa taifa lolote, wala wa ufalme wowote, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, au na mkono wa baba zangu; sembuse Mungu wenu atawaokoaje ninyi na mkono wangu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msidanganywe na Hezekia wala msishawishike kwa hayo. Msimwamini mtu huyu, kwa maana hapajatokea mungu wa taifa au mfalme yeyote aliyefaulu kuwakomboa watu wake kutoka mikononi mwa mfalme wa Ashuru, sembuse huyu Mungu wenu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sasa Hizikia asiwadanganye na kuwaponza ninyi kwa maneno kama hayo! Msimtegemee! Kwani hakuna mungu wo wote wa taifa au ufalme wo wote ulioweza kuwaponya watu wake mkononi mwangu wala mikononi mwa baba zangu. Sembuse Mungu wenu atawezaje kuwaponya mkononi mwangu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi sasa asiwadanganye Hezekia, wala asiwashawishi kwa hayo, wala msimwamini; kwa kuwa hapana mungu wa taifa lo lote, wala wa ufalme wo wote, aliyeweza kuwaokoa watu wake na mkono wangu, au na mkono wa baba zangu; sembuse Mungu wenu atawaokoaje ninyi na mkono wangu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musidanganywe na Hezekia wala musishawishiwe kwa hayo. Musimwamini mutu huyu, kwa maana hakujatokea mungu wa taifa au mufalme yeyote aliyeweza kuwakomboa watu wake kutoka mikono ya mufalme wa Asuria. Vile vile mungu wenu hataweza!”