2 Chronicles 32:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfalme mwenyewe aliandika barua akamtukana na kumdharau Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, akisema, “Kama vile ambavyo miungu ya mataifa mengine haikuweza kuwaokoa watu wao kutoka mikononi mwangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hataweza kuwaokoa watu wake.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mfalme pia aliandika barua akimtukana Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, na kusema haya dhidi yake: “Kama vile miungu ya mataifa ya nchi nyingine ilivyoshindwa kuwaokoa watu wao mkononi mwangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hataweza kuwaokoa watu wake kutoka mkononi mwangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena akaandika waraka, kumtukana Bwana, Mungu wa Israeli, na kumwambia, akisema, Kama vile miungu ya mataifa wa nchi isivyowaokoa watu wao na mkono wangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake na mkono wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfalme mwenyewe aliandika barua akamtukana na kumdharau Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, akisema, “Kama vile ambavyo miungu ya mataifa mengine haikuweza kuwaokoa watu wao kutoka mikononi mwangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hataweza kuwaokoa watu wake.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mfalme pia aliandika barua akimtukana BWANA, Mungu wa Israeli na kusema haya dhidi yake: “Kama vile miungu ya mataifa ya nchi nyingine ilivyoshindwa kuwaokoa watu wao mkononi mwangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hataweza kuwaokoa watu wake kutoka mkononi mwangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mfalme pia aliandika barua akimtukana bwana, Mungu wa Israeli na kusema haya dhidi yake: “Kama vile miungu ya mataifa ya nchi nyingine ilivyoshindwa kuwaokoa watu wao mkononi mwangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hataweza kuwaokoa watu wake kutoka mkononi mwangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena akaandika waraka, kumtukana BWANA, Mungu wa Israeli, na kumwambia, akisema, Kama vile miungu ya mataifa wa nchi isivyowaokoa watu wao na mkono wangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake na mkono wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfalme mwenyewe aliandika barua akamtukana na kumdharau Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, akisema, “Kama vile ambavyo miungu ya mataifa mengine haikuweza kuwaokoa watu wao kutoka mikononi mwangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hataweza kuwaokoa watu wake.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akaandika nazo barua za kumfyoza Bwana Mungu wa Isiraeli, akisema humo kwamba: Kama miungu ya mataifa ya nchi hizi isivyoweza kuwaponya watu wao mkononi mwangu, vivyo hivyo naye Mungu wa Hizikia hataweza kuwaponya watu wake mkononi mwangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena akaandika waraka, kumtukana BWANA, Mungu wa Israeli, na kumwambia, akisema, Kama vile miungu ya mataifa wa nchi isivyowaokoa watu wao na mkono wangu, vivyo hivyo Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake na mkono wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mufalme mwenyewe aliandika barua akamutukana na kumuzarau Yawe, Mungu wa Israeli, akisema: “Kama vile ambavyo miungu ya inchi zingine haikuweza kuwaokoa watu wao kutoka mikono yangu, vile vile mungu wa Hezekia hataweza kuwaokoa watu wake.”