2 Chronicles 32:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naye Mwenyezi-Mungu akatuma malaika, akaenda na kuwakatilia mbali mashujaa, wanajeshi, makamanda na maofisa katika kambi ya mfalme wa Ashuru. Basi, mfalme wa Ashuru akarejea nchini mwake amejawa aibu. Mara alipoingia ndani ya nyumba ya mungu wake, baadhi ya wanawe mwenyewe wakamuua papo hapo kwa upanga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Mwenyezi Mungu akamtuma malaika ambaye aliangamiza wapiganaji wote, na viongozi na maafisa katika kambi ya mfalme wa Ashuru. Kwa hiyo, mfalme wa Ashuru akarudi nchini mwake kwa aibu. Naye alipoenda katika hekalu la mungu wake, baadhi ya watoto wake mwenyewe wakamuua kwa upanga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Bwana akatuma malaika aliyewakatia mbali mashujaa wote, na majemadari, na maakida, matuoni mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake mwenye haya ya uso. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, wale waliotoka viunoni mwake mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naye Mwenyezi-Mungu akatuma malaika, akaenda na kuwakatilia mbali mashujaa, wanajeshi, makamanda na maofisa katika kambi ya mfalme wa Ashuru. Basi, mfalme wa Ashuru akarejea nchini mwake amejawa aibu. Mara alipoingia ndani ya nyumba ya mungu wake, baadhi ya wanawe mwenyewe wakamuua papo hapo kwa upanga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye BWANA akamtuma malaika ambaye aliangamiza wanaume wote wenye kupigana na viongozi na maafisa katika kambi ya mfalme wa Ashuru. Kwa hiyo, Mfalme wa Ashuru akarudi kwenye nchi yake mwenyewe kwa aibu. Naye alipokwenda katika hekalu la mungu wake, baadhi ya watoto wake walimkata na kumwua kwa upanga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye bwana akamtuma malaika ambaye aliangamiza wanajeshi wote, na viongozi na maafisa katika kambi ya mfalme wa Ashuru. Kwa hiyo, mfalme wa Ashuru akarudi nchini mwake kwa aibu. Naye alipokwenda katika hekalu la mungu wake, baadhi ya watoto wake wakamuua kwa upanga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye BWANA akatuma malaika aliyewakatilia mbali wapiganaji vita wote, na majemadari, na makamanda, kambini mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake kwa aibu. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, baadhi ya wanawe mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naye Mwenyezi-Mungu akatuma malaika, akaenda na kuwakatilia mbali mashujaa, wanajeshi, makamanda na maofisa katika kambi ya mfalme wa Ashuru. Basi, mfalme wa Ashuru akarejea nchini mwake amejawa aibu. Mara alipoingia ndani ya nyumba ya mungu wake, baadhi ya wanawe mwenyewe wakamuua papo hapo kwa upanga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana akatuma malaika wake, akaangamiza katika makambi ya mfalme wa Asuri mafundi wa vita wote waliokuwa wenye nguvu na wenye amri na wakuu, naye yeye hakuwa na budi kurudi kwao na kuuinamisha uso chini kwa soni. Alipoingia nyumbani mwa mungu wake, ndipo, wanawe wengine waliozaliwa naye mwenyewe walipomwua kwa upanga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye BWANA akatuma malaika aliyewakatia mbali mashujaa wote, na majemadari, na maakida, matuoni mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake mwenye haya ya uso. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, wale waliotoka viunoni mwake mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye Yawe akatuma malaika aliyewaua waaskari shujaa, majemadari na wakubwa katika kambi ya mufalme wa Asuria. Basi, mufalme wa Asuria akarudia katika inchi yake akijaa haya. Mara tu alipoingia ndani ya nyumba ya mungu wake, wana wake mwenyewe wakamwua palepale kwa upanga.