2 Chronicles 32:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa njia hii basi, Mwenyezi-Mungu akamwokoa mfalme Hezekia na wakazi wa Yerusalemu kutoka mkono wa Senakeribu mfalme wa Ashuru, na kutoka mkono wa maadui wake wote. Akawapa maisha ya amani na jirani zake wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Mwenyezi Mungu akamwokoa Hezekia na watu wa Yerusalemu kutoka mkononi mwa Senakeribu mfalme wa Ashuru na kutoka mikononi mwa wengine wote. Mwenyezi Mungu akawapa amani pande zote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndivyo Bwana alivyomwokoa Hezekia, na wenyeji wa Yerusalemu, na mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na mikononi mwa wote, akawaongoza pande zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa njia hii basi, Mwenyezi-Mungu akamwokoa mfalme Hezekia na wakazi wa Yerusalemu kutoka mkono wa Senakeribu mfalme wa Ashuru, na kutoka mkono wa maadui wake wote. Akawapa maisha ya amani na jirani zake wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo BWANA akamwokoa Hezekia na watu wa Yerusalemu kutoka mkononi mwa Senakeribu mfalme wa Ashuru na kutoka mikononi mwa wengine wote. BWANA akawastarehesha kila upande.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo bwana akamwokoa Hezekia na watu wa Yerusalemu kutoka mkononi mwa Senakeribu mfalme wa Ashuru na kutoka mikononi mwa wengine wote. bwana akawastarehesha kila upande.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndivyo BWANA alivyomwokoa Hezekia, na wenyeji wa Yerusalemu kutoka katika mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na mikononi mwa wote, akawaongoza pande zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa njia hii basi, Mwenyezi-Mungu akamwokoa mfalme Hezekia na wakazi wa Yerusalemu kutoka mkono wa Senakeribu mfalme wa Ashuru, na kutoka mkono wa maadui wake wote. Akawapa maisha ya amani na jirani zake wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, Bwana alivyomwokoa Hizikia na wenyeji wa Yerusalemu mkononi mwa Saniheribu, mfalme wa Wasuri, namo mikononi mwao wote wengine akiwalinda pande zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndivyo BWANA alivyomwokoa Hezekia, na wenyeji wa Yerusalemu, na mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na mikononi mwa wote, akawaongoza pande zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa njia hii basi, Yawe akamwokoa mufalme Hezekia na wakaaji wa Yerusalema kutoka mukono wa Saniharibu mufalme wa Asuria, na kutoka mukono wa waadui zake wote. Akawapa maisha ya amani na wajirani zao wote.