2 Chronicles 32:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Hezekia hakumtolea Mwenyezi-Mungu shukrani kwa hayo yote aliyomtendea kwa kuwa moyo wake ulikuwa umejaa majivuno. Hii ilisababisha kutaabika kwa Yuda na Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini moyo wa Hezekia ukajaa majivuno na hakuonesha itikio kwa wema aliotendewa, kwa hiyo ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ikawa juu yake na juu ya Yuda na Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini kadiri alivyofadhiliwa Hezekia hakumrudishia vivyo; kwa kuwa moyo wake ulitukuka; kwa hiyo ikawako hasira juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Hezekia hakumtolea Mwenyezi-Mungu shukrani kwa hayo yote aliyomtendea kwa kuwa moyo wake ulikuwa umejaa majivuno. Hii ilisababisha kutaabika kwa Yuda na Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini moyo wa Hezekia ukajaa majivuno na hakuonyesha itikio kwa wema aliotendewa, kwa hiyo ghadhabu ya BWANA ikawa juu yake na juu ya Yuda na Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini moyo wa Hezekia ukajaa majivuno na hakuonyesha itikio kwa wema aliotendewa, kwa hiyo ghadhabu ya bwana ikawa juu yake na juu ya Yuda na Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Walakini Hezekia hakuwa na shukrani kadiri alivyofadhiliwa; kwa kuwa moyo wake ulijawa na kiburi; kwa hiyo ikawako hasira juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Hezekia hakumtolea Mwenyezi-Mungu shukrani kwa hayo yote aliyomtendea kwa kuwa moyo wake ulikuwa umejaa majivuno. Hii ilisababisha kutaabika kwa Yuda na Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Hizikia hakuyarudisha hayo mema aliyofanyiziwa, kwa kuwa moyo wake ulijikuza. Kwa hiyo makali ya Bwana yakaja kumkalia yeye, hata Wayuda na Wayerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini kadiri alivyofadhiliwa Hezekia hakumrudishia vivyo; kwa kuwa moyo wake ulitukuka; kwa hiyo ikawako hasira juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Hezekia hakumutolea Yawe shukrani kwa yale yote aliyomutendea kwa sababu moyo wake ulikuwa umejaa majivuno. Hii ikasababisha kutaabika kwa inchi ya Yuda na Yerusalema.