2 Chronicles 32:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo ghadhabu ikawa juu yake, juu ya Yuda na juu ya Yerusalemu. Hatimaye Hezekia alinyenyekea akaacha kuwa na moyo uliojaa majivuno; yeye na wakazi wa Yerusalemu walijinyenyekesha kwa hiyo ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu haikuwajia wakati Hezekia alipokuwa hai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Hezekia akatubu kwa ajili ya kiburi cha moyo wake, kama walivyofanya watu wa Yerusalemu, kwa hiyo ghadhabu ya Mwenyezi Mungu haikuja juu yao katika siku za Hezekia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata hivyo Hezekia akajinyenyekeza kwa ajili ya huku kutukuka kwa moyo wake, yeye na wenyeji wa Yerusalemu, hata haikuwajia hasira ya Bwana siku za Hezekia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo ghadhabu ikawa juu yake, juu ya Yuda na juu ya Yerusalemu. Hatimaye Hezekia alinyenyekea akaacha kuwa na moyo uliojaa majivuno; yeye na wakazi wa Yerusalemu walijinyenyekesha kwa hiyo ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu haikuwajia wakati Hezekia alipokuwa hai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Hezekia akatubu kwa ajili ya kiburi cha moyo wake, kama walivyofanya watu wa Yerusalemu, kwa hiyo ghadhabu ya BWANA haikuja juu yao katika siku za Hezekia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Hezekia akatubu kwa ajili ya kiburi cha moyo wake, kama walivyofanya watu wa Yerusalemu, kwa hiyo ghadhabu ya bwana haikuja juu yao katika siku za Hezekia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata hivyo Hezekia akajinyenyekeza kwa ajili ya kiburi cha moyo wake, yeye na wenyeji wa Yerusalemu, hata haikuwajia hasira ya BWANA siku za Hezekia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo ghadhabu ikawa juu yake, juu ya Yuda na juu ya Yerusalemu. Hatimaye Hezekia alinyenyekea akaacha kuwa na moyo uliojaa majivuno; yeye na wakazi wa Yerusalemu walijinyenyekesha kwa hiyo ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu haikuwajia wakati Hezekia alipokuwa hai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Hizikia kwa hivyo, moyo wake ulivyojikuza, akajinyenyekeza tena yeye pamoja na wenyeji wa Yerusalemu; kwa sababu hii makali ya Bwana hayakuwatokea siku za Hizikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata hivyo Hezekia akajinyenyekeza kwa ajili ya huku kutukuka kwa moyo wake, yeye na wenyeji wa Yerusalemu, hata haikuwajia hasira ya BWANA siku za Hezekia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo kasirani ikakuwa juu yake, juu ya inchi ya Yuda na juu ya Yerusalema. Kisha Hezekia akanyenyekea akaacha kuwa na moyo uliojaa majivuno, yeye na wakaaji wa Yerusalema wakajinyenyekeza; kwa hiyo kasirani ya Yawe haikuwafikia wakati wa utawala wa Hezekia.