2 Chronicles 32:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hezekia alifariki dunia na kuzikwa kwenye sehemu ya juu ya makaburi ya wafalme. Watu wote wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu walimtolea heshima kuu wakati wa kifo chake, naye Manase, mwanawe, akatawala mahali pake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hezekia akalala na baba zake na akazikwa kwenye kilima mahali yalipo makaburi ya wazao wa Daudi. Yuda wote na watu wa Yerusalemu wakamheshimu alipofariki. Naye Manase mwanawe akawa mfalme baada yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hezekia akalala na babaze, wakamzika mahali pa kupandia makaburi ya wana wa Daudi; nao Yuda wote na wenyeji wa Yerusalemu wakamfanyia heshima alipokufa. Na Manase mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hezekia alifariki dunia na kuzikwa kwenye sehemu ya juu ya makaburi ya wafalme. Watu wote wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu walimtolea heshima kuu wakati wa kifo chake, naye Manase, mwanawe, akatawala mahali pake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hezekia akalala na baba zake na akazikwa kwenye kilima mahali yalipo makaburi ya wazao wa Daudi. Yuda wote na watu wa Yerusalemu wakamheshimu alipokufa. Naye Manase mwanawe akaingia mahali pake kuwa mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hezekia akalala na baba zake na akazikwa kwenye kilima mahali yalipo makaburi ya wazao wa Daudi. Yuda wote na watu wa Yerusalemu wakamheshimu alipofariki. Naye Manase mwanawe akawa mfalme baada yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hezekia akalala na babaze, wakamzika mahali pa kupandia makaburi ya wana wa Daudi; nao Yuda wote na wenyeji wa Yerusalemu wakamfanyia heshima alipokufa. Na Manase mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hezekia alifariki dunia na kuzikwa kwenye sehemu ya juu ya makaburi ya wafalme. Watu wote wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu walimtolea heshima kuu wakati wa kifo chake, naye Manase, mwanawe, akatawala mahali pake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hizikia alipokwenda kulala na baba zake, wakamzika pa kupandia penye makaburi ya wana wa Dawidi; Wayuda wote na wenyeji wa Yerusalemu wakamheshimu sana, alipokufa. Naye mwanawe Manase akawa mfalme mahali pake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hezekia akalala na babaze, wakamzika mahali pa kupandia makaburi ya wana wa Daudi; nao Yuda wote na wenyeji wa Yerusalemu wakamfanyia heshima alipokufa. Na Manase mwanawe akatawala mahali pake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hezekia akakufa na kuzikwa kwenye sehemu ya juu ya makaburi ya wafalme. Watu wote wa inchi ya Yuda na wakaaji wa Yerusalema wakamutolea heshima kubwa wakati wa kifo chake, naye Manase, mwana wake, akatawala pahali pake.