2 Chronicles 32:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ili kuuhami mji, mfalme Hezekia alipiga moyo konde, akajenga upya ukuta wote uliokuwa umebomoka, na juu yake akajenga minara. Upande wa nje, akajenga ukuta mwingine wa pili, na akaiimarisha sehemu iliyoitwa Milo katika mji wa Daudi. Zaidi ya hayo alitengeneza silaha na ngao kwa wingi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hezekia akafanya kazi kwa bidii kukarabati sehemu zote zilizokuwa zimebomoka za ukuta na kujenga minara juu yake. Akajenga ukuta mwingine nje ya ule uliokuwako, na kuimarisha Milo katika Mji wa Daudi. Akatengeneza pia silaha nyingi na ngao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akapiga moyo konde, akaujenga ukuta wote uliobomoka, akauinua sawa na minara, na ukuta wa pili nje, akaongeza nguvu ya Milo, katika mji wa Daudi, akafanya silaha na ngao tele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ili kuuhami mji, mfalme Hezekia alipiga moyo konde, akajenga upya ukuta wote uliokuwa umebomoka, na juu yake akajenga minara. Upande wa nje, akajenga ukuta mwingine wa pili, na akaiimarisha sehemu iliyoitwa Milo katika mji wa Daudi. Zaidi ya hayo alitengeneza silaha na ngao kwa wingi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hezekia akafanya kazi kwa bidii kukarabati sehemu zote zilizokuwa zimebomoka za ukuta na kujenga minara juu yake. Akajenga ukuta mwingine nje ya ule uliokuwepo na kuimarisha milo katika Mji wa Daudi. Akatengeneza pia silaha nyingi na ngao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hezekia akafanya kazi kwa bidii kukarabati sehemu zote zilizokuwa zimebomoka za ukuta na kujenga minara juu yake. Akajenga ukuta mwingine nje ya ule uliokuwepo na kuimarisha Milo katika Mji wa Daudi. Akatengeneza pia silaha nyingi na ngao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hezekia akapiga moyo konde, akaujenga ukuta wote uliobomoka, akauinua sawa na minara, na ukuta wa pili nje, akaongeza nguvu ya Milo, katika mji wa Daudi, akafanya silaha na ngao tele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ili kuuhami mji, mfalme Hezekia alipiga moyo konde, akajenga upya ukuta wote uliokuwa umebomoka, na juu yake akajenga minara. Upande wa nje, akajenga ukuta mwingine wa pili, na akaiimarisha sehemu iliyoitwa Milo katika mji wa Daudi. Zaidi ya hayo alitengeneza silaha na ngao kwa wingi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akakaza kuutengeneza ukuta wote wa boma na kuujenga tena hapo, ulipobomoka, hata minara akaipandisha kwenda juu zaidi, nao ukuta wa pili wa nje akaujenga tena, hata ngome ya mji wa Dawidi akaitia nguvu, akatengeneza mata na ngao nyingi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akapiga moyo konde, akaujenga ukuta wote uliobomoka, akauinua sawa na minara, na ukuta wa pili nje, akaongeza nguvu ya Milo, katika mji wa Daudi, akafanya silaha na ngao tele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hezekia akajitia moyo, akajenga upya ukuta wote uliokuwa umebomoka, na juu yake akajenga minara. Upande wa inje, akajenga ukuta mwingine wa pili, na akaiimarisha uwanja wa Milo katika muji wa Daudi. Zaidi ya hayo akatengeneza silaha na ngao kwa wingi.