2 Chronicles 33:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maana alirekebisha mahali pa kuabudia miungu mingine palipokuwa pamebomolewa na Hezekia baba yake; akajenga madhabahu za kuabudia Mabaali, akatengeneza na sanamu za Maashera. Isitoshe, aliabudu vitu vyote vya mbinguni na kuvitumikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia ambapo Hezekia baba yake, alikuwa amepabomoa. Pia akasimamisha madhabahu za Mabaali na nguzo za Maashera. Akayasujudia majeshi yote ya angani na kuyaabudu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopabomoa Hezekia babaye; akazisimamisha madhabahu za mabaali, akafanya na sanamu za maashera, akaabudu jeshi lote la mbinguni, na kulitumikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maana alirekebisha mahali pa kuabudia miungu mingine palipokuwa pamebomolewa na Hezekia baba yake; akajenga madhabahu za kuabudia Mabaali, akatengeneza na sanamu za Maashera. Isitoshe, aliabudu vitu vyote vya mbinguni na kuvitumikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo Hezekia baba yake, alikuwa amepabomoa, pia akasimamisha madhabahu za Mabaali na nguzo za Maashera. Akalisujudia jeshi lote la vitu vya angani na kuliabudu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akajenga upya mahali pa juu pa kuabudia miungu ambapo Hezekia baba yake, alikuwa amepabomoa, pia akasimamisha madhabahu za Mabaali na nguzo za Maashera. Akalisujudia jeshi lote la angani na kuliabudu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopabomoa Hezekia babaye; akazisimamisha madhabahu za Mabaali, akafanya sanamu za Maashera, akaabudu jeshi lote la mbinguni, na kulitumikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maana alirekebisha mahali pa kuabudia miungu mingine palipokuwa pamebomolewa na Hezekia baba yake; akajenga madhabahu za kuabudia Mabaali, akatengeneza na sanamu za Maashera. Isitoshe, aliabudu vitu vyote vya mbinguni na kuvitumikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akavijenga tena vijumba vya kutambikia vilimani, baba yake Hizikia alivyovibomoa, akaweka hata meza za kutambikia Mabaali, akatengeneza navyo vinyago vya Ashera, akaviangukia vikosi vyote vya mbinguni na kuvitumikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopabomoa Hezekia babaye; akazisimamisha madhabahu za mabaali, akafanya na sanamu za maashera, akaabudu jeshi lote la mbinguni, na kulitumikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana alijenga tena pahali pa kuabudia miungu mingine palipokuwa pamebomolewa na baba yake Hezekia; akajenga mazabahu za kuabudia Mabali, na kutengeneza sanamu za Ashera. Vilevile, aliabudu jeshi la mbinguni na kulitumikia.