2 Chronicles 33:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pia aliwatoa wanawe kama sadaka ya kuteketeza katika bonde la mwana wa Hinomu. Alipiga ramli, alibashiri na alitumia hirizi; hata alishirikiana na waaguzi wa mizimu na wachawi. Alitenda maovu mengi mbele ya Mwenyezi-Mungu, akamkasirisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawatoa kafara watoto wake kwa kuwapitishia motoni katika Bonde la Ben-Hinomu; akafanya ulozi, uaguzi, na uchawi, akatafuta ushauri kwa wenye pepo wa utambuzi na wenye kuwasiliana na mizimu. Akafanya maovu mengi machoni pa Mwenyezi Mungu, akaichochea hasira yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena akawapitisha wanawe motoni katika bonde la mwana wa Hinomu; akatazama bao, akabashiri, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pia aliwatoa wanawe kama sadaka ya kuteketeza katika bonde la mwana wa Hinomu. Alipiga ramli, alibashiri na alitumia hirizi; hata alishirikiana na waaguzi wa mizimu na wachawi. Alitenda maovu mengi mbele ya Mwenyezi-Mungu, akamkasirisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawatoa wanawe kuwa kafara kwa kuwapitisha katika moto katika Bonde la Hinomu, akafanya ulozi, uaguzi na uchawi, akataka ushauri kwa wenye pepo wa utambuzi na wenye kuwasiliana na mizimu. Akafanya maovu mengi machoni pa BWANA, akaichochea hasira yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawatoa wanawe kuwa kafara kwa kuwapitisha katika moto katika Bonde la Ben-Hinomu, akafanya ulozi, uaguzi na uchawi, akataka ushauri kwa wenye pepo wa utambuzi na wenye kuwasiliana na mizimu. Akafanya maovu mengi machoni pa bwana, akaichochea hasira yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena akawapitisha wanawe motoni katika bonde la mwana wa Hinomu; akatazama bao, akabashiri, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa BWANA, na kumkasirisha.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pia aliwatoa wanawe kama sadaka ya kuteketeza katika bonde la mwana wa Hinomu. Alipiga ramli, alibashiri na alitumia hirizi; hata alishirikiana na waaguzi wa mizimu na wachawi. Alitenda maovu mengi mbele ya Mwenyezi-Mungu, akamkasirisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata wanawe akawatumia kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa motoni katika Bonde la Bin-Hinomu; tena akaagulia mawingu, akapiga bao, tena akafanya uchawi, akatumia nao wakweza mizimu na wapunga pepo; akazidi kuyafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana, amkasirishe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena akawapitisha wanawe motoni katika bonde la mwana wa Hinomu; akatazama bao, akabashiri, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa BWANA, hata kumkasirisha.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na aliwatoa wana wake kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto katika bonde la mwana wa Hinomu. Alipiga ramuli, aliaguza na alitumia hirizi; hata alishirikiana na waaguzi wanaosemezana na mizimu na wachawi. Alitenda maovu mengi mbele ya Yawe, akamukasirikisha.