2 Chronicles 33:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nayo sanamu aliyoitengeneza, aliiweka katika nyumba ya Mungu mahali alipopazungumzia, mbele ya Daudi na Solomoni mwanawe: “Katika nyumba hii na katika Yerusalemu kati ya makabila kumi na mawili ya Israeli, ndipo mahali nitakapoabudiwa milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akachukua ile sanamu aliyoichonga na kuiweka katika Hekalu la Mungu ambalo Mungu alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Sulemani, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu, mji niliouchagua kutoka makabila yote ya Israeli, nitaliweka Jina langu milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaiweka sanamu ya kuchonga aliyoifanya, katika nyumba ya Mungu ambayo Mungu alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nayo sanamu aliyoitengeneza, aliiweka katika nyumba ya Mungu mahali alipopazungumzia, mbele ya Daudi na Solomoni mwanawe: “Katika nyumba hii na katika Yerusalemu kati ya makabila kumi na mawili ya Israeli, ndipo mahali nitakapoabudiwa milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akachukua ile sanamu aliyoichonga akaiweka katika Hekalu la BWANA ambalo Mungu alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Solomoni, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu niliouchagua kutoka kabila zote za Israeli, nitaliweka Jina langu milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akachukua ile sanamu aliyoichonga na kuiweka katika Hekalu la mungu ambalo Mungu alikuwa amemwambia Daudi na mwanawe Sulemani, “Katika Hekalu hili na katika Yerusalemu niliouchagua kutoka kabila zote za Israeli, nitaliweka Jina langu milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaiweka sanamu ya kuchonga aliyoifanya, katika nyumba ya Mungu ambayo Mungu alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nayo sanamu aliyoitengeneza, aliiweka katika nyumba ya Mungu mahali alipopazungumzia, mbele ya Daudi na Solomoni mwanawe: “Katika nyumba hii na katika Yerusalemu kati ya makabila kumi na mawili ya Israeli, ndipo mahali nitakapoabudiwa milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nacho kinyago cha kuchora, alichokitengeneza, akakiweka katika Nyumba ya Mungu, ambayo Mungu alimwambia Dawidi na mwanawe Salomo: Humu Nyumbani namo Yerusalemu, niliouchagua katika mashina yote ya Isiraeli, nitalikalisha Jina langu kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaiweka sanamu ya kuchonga aliyoifanya, katika nyumba ya Mungu ambayo Mungu alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nayo sanamu aliyotengeneza, akaiweka katika nyumba ya Mungu ambayo aliizungumuzia, mbele ya Daudi na mwana wake Solomono: “Katika nyumba hii na katika Yerusalema kati ya makabila kumi na mawili ya Israeli, ndipo pahali nitakapoabudiwa milele.