2 Chronicles 34:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati walipokuwa wanashughulika na utoaji wa fedha zilizokuwa zimeletwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, kuhani Hilkia alipata Kitabu cha Sheria ya Mwenyezi-Mungu iliyotolewa kwa mkono wa Mose.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati walikuwa wakizitoa nje fedha zilizokuwa zimetolewa kwenye Hekalu la Mwenyezi Mungu, kuhani Hilkia akakipata kile Kitabu cha Torati ya Mwenyezi Mungu kilichokuwa kimetolewa kwa mkono wa Musa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao walipotoa ile fedha iliyoletwa nyumbani mwa Bwana, Hilkia kuhani akakiona kitabu cha torati ya Bwana iliyotolewa kwa mkono wa Musa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati walipokuwa wanashughulika na utoaji wa fedha zilizokuwa zimeletwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, kuhani Hilkia alipata Kitabu cha Sheria ya Mwenyezi-Mungu iliyotolewa kwa mkono wa Mose.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati walipokuwa wakizitoa nje zile fedha zilizokuwa zimetolewa kwenye Hekalu la BWANA kuhani Hilkia akakipata kile Kitabu cha Sheria ya BWANA kilichokua kimetolewa kwa mkono wa Mose.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati walikuwa wakizitoa nje fedha zilizokuwa zimetolewa kwenye Hekalu la bwana, kuhani Hilkia akakipata kile Kitabu cha Torati ya bwana kilichokua kimetolewa kwa mkono wa Musa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao walipotoa ile fedha iliyoletwa nyumbani mwa BWANA, Hilkia kuhani akakiona kitabu cha Torati ya BWANA iliyotolewa kwa mkono wa Musa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati walipokuwa wanashughulika na utoaji wa fedha zilizokuwa zimeletwa katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, kuhani Hilkia alipata Kitabu cha Sheria ya Mwenyezi-Mungu iliyotolewa kwa mkono wa Mose.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipozitoa zile fedha zilizopelekwa Nyumbani mwa Bwana, ndipo, mtambikaji Hilkia alipokiona kitabu cha Maonyo ya Bwana, aliyopewa Mose.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao walipotoa ile fedha iliyoletwa nyumbani mwa BWANA, Hilkia kuhani akakiona kitabu cha torati ya BWANA iliyotolewa kwa mkono wa Musa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati walipokuwa wakitoa inje feza zilizokuwa zimeletwa katika nyumba ya Yawe, kuhani Hilkia akapata kitabu cha Sheria ya Yawe iliyotolewa kwa mukono wa Musa.