2 Chronicles 34:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Nendeni mkatafute shauri kutoka kwa Mwenyezi-Mungu kwa niaba yangu na watu ambao wamebaki katika Israeli na Yuda, kuhusu maneno yaliyomo katika kitabu kilichopatikana. Kwa sababu ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu imetuangukia, maana babu zetu hawakushika neno la Mwenyezi-Mungu, wala kufanya yaliyoandikwa humo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nendeni mkamuulize Mwenyezi Mungu kwa ajili yangu na kwa ajili ya mabaki waliosalia katika Israeli na Yuda, kuhusu yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya Mwenyezi Mungu iliyomwagwa juu yetu ni kubwa mno kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la Mwenyezi Mungu wala hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa katika Kitabu hiki.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nendeni, mkamwulize Bwana kwa ajili yangu, na kwa hao waliosalia wa Israeli na wa Yuda, katika habari za maneno ya kitabu kilichoonekana; maana ghadhabu ya Bwana ni nyingi iliyomwagika juu yetu, kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la Bwana, kutenda sawasawa na yote yaliyoandikwa kitabuni humo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Nendeni mkatafute shauri kutoka kwa Mwenyezi-Mungu kwa niaba yangu na watu ambao wamebaki katika Israeli na Yuda, kuhusu maneno yaliyomo katika kitabu kilichopatikana. Kwa sababu ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu imetuangukia, maana babu zetu hawakushika neno la Mwenyezi-Mungu, wala kufanya yaliyoandikwa humo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nendeni mkamwulize BWANA kwa ajili yangu na kwa ajili ya mabaki walioko Israeli na Yuda kuhusu haya yaliyoandikwa katika kitabu hiki ambacho kimeonekana hekaluni. Hasira ya BWANA ni kubwa mno ambayo imemwagwa juu yetu kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la BWANA wala hawakutenda sawasawa na yale yote yaliyoandikwa katika Kitabu hiki.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nendeni mkamuulize bwana kwa ajili yangu na kwa ajili ya mabaki walioko Israeli na Yuda kuhusu yale yaliyoandikwa ndani ya kitabu hiki ambacho kimepatikana. Hasira ya bwana ni kubwa mno ambayo imemwagwa juu yetu kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la bwana wala hawajatenda kulingana na yale yote yaliyoandikwa katika Kitabu hiki.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nendeni, mkamwulize BWANA kwa ajili yangu, na kwa hao waliosalia wa Israeli na wa Yuda, kuhusu habari za maneno ya kitabu kilichoonekana; maana ghadhabu ya BWANA ni nyingi iliyomwagika juu yetu, kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la BWANA, kutenda sawasawa na yote yaliyoandikwa kitabuni humo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Nendeni mkatafute shauri kutoka kwa Mwenyezi-Mungu kwa niaba yangu na watu ambao wamebaki katika Israeli na Yuda, kuhusu maneno yaliyomo katika kitabu kilichopatikana. Kwa sababu ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu imetuangukia, maana babu zetu hawakushika neno la Mwenyezi-Mungu, wala kufanya yaliyoandikwa humo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nendeni kuniulizia Bwana mimi na masao ya Waisiraeli na ya Wayuda kwa ajili ya maneno ya hiki kitabu kilichooneka, kwani makali ya Bwana yenye moto ni makuu, nayo humwagika kwetu, kwa kuwa baba zetu hawakulishika Neno la Bwana na kuyafanya yote yaliyoandikwa humu kitabuni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nendeni, mkamwulize BWANA kwa ajili yangu, na kwa hao waliosalia wa Israeli na wa Yuda, katika habari za maneno ya kitabu kilichoonekana; maana ghadhabu ya BWANA ni nyingi iliyomwagika juu yetu, kwa sababu baba zetu hawakulishika neno la BWANA, kutenda sawasawa na yote yaliyoandikwa kitabuni humo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mwende mutafute shauri kutoka kwa Yawe kwa ajili yangu na kwa ajili ya watu ambao wamebaki katika Israeli na Yuda, juu ya maneno yanayokuwa katika kitabu kilichopatikana. Kwa sababu kasirani ya Yawe imetuangukia maana babu zetu hawakushika Neno la Yawe wala kufanya yaliyoandikwa humo.”