2 Chronicles 34:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa sababu wameniacha mimi na kufukizia miungu mingine ubani ili wanikasirishe sana kwa kazi zote za mikono yao, basi ghadhabu yangu itamwagika juu ya mahali hapa wala haitatulizwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu wameniacha na kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kunighadhibisha kwa kazi yote ya mikono yao, hivyo hasira yangu itamwagwa mahali hapa, wala haitatulizwa.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa sababu wameniacha mimi, na kuifukizia uvumba miungu mingine, ili wanikasirishe mimi kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo ghadhabu yangu imemwagika juu ya mahali hapa, wala isizimike.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa sababu wameniacha mimi na kufukizia miungu mingine ubani ili wanikasirishe sana kwa kazi zote za mikono yao, basi ghadhabu yangu itamwagika juu ya mahali hapa wala haitatulizwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu wameniacha mimi na kufukiza uvumba kwa miungu mingine ili waichochee hasira yangu kwa kazi yote ya mikono yao, hivyo hasira yangu itamwagwa juu ya mahali hapa, wala haitatulizwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa sababu wameniacha mimi na kufukiza uvumba kwa miungu mingine na kunighadhibisha kwa kazi yote ya mikono yao, hivyo hasira yangu itamwagwa juu ya mahali hapa, wala haitatulizwa.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa sababu wameniacha mimi, na kuifukizia uvumba miungu mingine, ili wanikasirishe mimi kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo ghadhabu yangu imemwagika juu ya mahali hapa, wala isizimike.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa sababu wameniacha mimi na kufukizia miungu mingine ubani ili wanikasirishe sana kwa kazi zote za mikono yao, basi ghadhabu yangu itamwagika juu ya mahali hapa wala haitatulizwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kwa kuwa wameniacha, wakavukizia miungu mingine, wanikasirishe kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo makali yangu yenye moto yatamwagwa hapa, wala hayatazimika.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa sababu wameniacha mimi, na kuifukizia uvumba miungu mingine, ili wanikasirishe mimi kwa matendo yote ya mikono yao; kwa hiyo ghadhabu yangu imemwagika juu ya mahali hapa, wala isizimike.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa sababu wameniacha mimi na kufukizia miungu mingine ubani kusudi wanikasirikishe sana kwa kazi zote za mikono yao, basi kasirani yangu itamwagika juu ya pahali hapa wala haitatulizwa.