2 Chronicles 34:27 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa kuwa umetubu na kunyenyekea mbele yangu, hata umerarua mavazi yako na kulia uliposikia maneno yangu dhidi ya mahali hapa, na dhidi ya wakazi wake, na umejinyenyekesha mbele yangu, nami pia nimekusikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa moyo wako ulikuwa msikivu na ulijinyenyekeza mbele za Mungu uliposikia kile nilichosema dhidi ya mahali hapa na watu wake na kwa sababu ulijinyenyekeza mbele zangu na uliyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe umejinyenyekeza mbele ya Mungu, uliposikia maneno yake juu ya mahali hapa, na juu ya wakaao, ukajinyenyekeza mbele zangu, na kuyararua mavazi yako, na kulia mbele zangu; mimi nami nimekusikia, asema Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwa kuwa umetubu na kunyenyekea mbele yangu, hata umerarua mavazi yako na kulia uliposikia maneno yangu dhidi ya mahali hapa, na dhidi ya wakazi wake, na umejinyenyekesha mbele yangu, nami pia nimekusikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa sababu moyo wako ulikuwa mwepesi kusikia, nawe ukajinyenyekeza mbele za Mungu wakati uliposikia kile alichokisema dhidi ya mahali hapa na watu wake na kwa sababu ulijinyenyekeza mbele zangu ukararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa moyo wako ulikuwa msikivu na ulijinyenyekeza mbele za Mungu uliposikia kile nilichosema dhidi ya mahali hapa na watu wake na kwa sababu ulijinyenyekeza mbele zangu na uliyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe umejinyenyekeza mbele ya Mungu, uliposikia maneno yake juu ya mahali hapa, na juu ya wakazi wake, ukajinyenyekeza mbele zangu, na kuyararua mavazi yako, na kulia mbele zangu; mimi nami nimekusikia, asema BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa kuwa umetubu na kunyenyekea mbele yangu, hata umerarua mavazi yako na kulia uliposikia maneno yangu dhidi ya mahali hapa, na dhidi ya wakazi wake, na umejinyenyekesha mbele yangu, nami pia nimekusikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
moyo wako umelegea, ukajinyenyekeza mbele ya Mungu papo hapo ulipoyasikia maneno yake, aliyoyasema ya mahali hapa na ya wenyeji wake, ukajinyenyekeza kweli mbele yangu na kuyararua mavazi yako na kunililia mimi, basi, kwa hiyo mimi nami nimekusikia; ndivyo, asemavyo Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kuwa moyo wako ulikuwa mwororo, nawe umejinyenyekeza mbele ya Mungu, uliposikia maneno yake juu ya mahali hapa, na juu ya wakaao, ukajinyenyekeza mbele zangu, na kuyararua mavazi yako, na kulia mbele zangu; mimi nami nimekusikia, asema BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kwa sababu umetubu na kunyenyekea mbele yangu, hata umepasua nguo yako na kulia uliposikia maneno yangu juu ya pahali hapa, na juu ya wakaaji wake, na umejinyenyekeza mbele yangu, nami vilevile nimekusikia. –Ni ujumbe wa Yawe.–