2 Chronicles 34:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Katika mwaka wa nne wa utawala wake, mfalme Yosia, akiwa bado kijana, alianza kumwabudu Mungu wa Daudi, baba yake. Baadaye alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili alianza kuisafisha Yuda na Yerusalemu kwa kuharibu mahali pa kuabudia miungu mingine, sanamu za Ashera, na sanamu nyinginezo za kuchonga na za kusubu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa nane wa utawala wake, alipokuwa angali bado mdogo, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi baba yake. Katika mwaka wake wa kumi na mbili alianza kutakasa mahali pa juu pa kuabudia pa Yuda na Yerusalemu, akiondoa nguzo za Ashera, sanamu za kuchonga, na sanamu za kusubu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa katika mwaka wa nane wa kutawala kwake, naye akali mchanga, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi babaye; hata katika mwaka wa kumi na mbili akaanza kusafisha Yuda na Yerusalemu kwa kuondoa mahali pa juu, na kwa kuondoa maashera, na sanamu za kuchora, nazo za kusubu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Katika mwaka wa nne wa utawala wake, mfalme Yosia, akiwa bado kijana, alianza kumwabudu Mungu wa Daudi, baba yake. Baadaye alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili alianza kuisafisha Yuda na Yerusalemu kwa kuharibu mahali pa kuabudia miungu mingine, sanamu za Ashera, na sanamu nyinginezo za kuchonga na za kusubu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa nane wa utawala wake, alipokuwa angali bado mdogo, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi baba yake. Katika mwaka wake wa kumi na mbili alianza kusafisha mahali pa juu pa kuabudia miungu pa Yuda na Yerusalemu, akiondoa nguzo za Ashera, sanamu za kuchonga na vinyago vya kusubu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa nane wa utawala wake, alipokuwa angali bado mdogo, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi baba yake. Katika mwaka wake wa kumi na mbili alianza kusafisha mahali pa juu pa kuabudia miungu pa Yuda na Yerusalemu, akiondoa nguzo za Ashera, sanamu za kuchonga na vinyago vya kusubu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa katika mwaka wa nane wa kutawala kwake, naye akiwa bado mchanga, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi babaye; hata katika mwaka wa kumi na mbili akaanza kusafisha Yuda na Yerusalemu kwa kuondoa mahali pa juu, na kwa kuondoa Maashera, na sanamu za kuchonga, na za kusubu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Katika mwaka wa nne wa utawala wake, mfalme Yosia, akiwa bado kijana, alianza kumwabudu Mungu wa Daudi, baba yake. Baadaye alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili alianza kuisafisha Yuda na Yerusalemu kwa kuharibu mahali pa kuabudia miungu mingine, sanamu za Ashera, na sanamu nyinginezo za kuchonga na za kusubu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa nane wa ufalme wake, yeye alipokuwa akingali mvulana, alianza kumtafuta Mungu wa baba yake Dawidi; tena katika mwaka wa kumi na mbili alianza kuitakasa nchi ya Yuda na mji wa Yerusalemu na kuyaondoa matambiko ya vilimani na miti ya Ashera na vinyago vingine vya kuchonga navyo vilivyoyeyushwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa katika mwaka wa nane wa kutawala kwake, naye akali mchanga, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi babaye; hata katika mwaka wa kumi na mbili akaanza kusafisha Yuda na Yerusalemu kwa kuondoa mahali pa juu, na kwa kuondoa maashera, na sanamu za kuchora, nazo za kusubu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa ine wa utawala wake, mufalme Yosia, akiwa bado kijana, alianza kumwabudu Mungu wa Daudi, babu yake. Kisha alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili alianza kusafisha inchi ya Yuda na Yerusalema kwa kuharibu pahali pa kutambikia miungu mingine, sanamu za Ashera, na sanamu zingine za kuchonga na za kuyeyusha.