2 Chronicles 34:32 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena aliwafanya wote waliokuwa katika Yerusalemu na katika Benyamini kuzingatia agano. Nao wakazi wa Yerusalemu waliishi kwa kufuata agano la Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo akamtaka kila mmoja katika Yerusalemu na Benyamini kuweka ahadi zao wenyewe kwa hilo agano, watu wa Yerusalemu wakafanya hivyo kwa kufuata agano la Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawafanya wote walioonekana katika Yerusalemu na Benyamini walikubali. Na wenyeji wa Yerusalemu wakafanya sawasawa na agano la Mungu, Mungu wa baba zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena aliwafanya wote waliokuwa katika Yerusalemu na katika Benyamini kuzingatia agano. Nao wakazi wa Yerusalemu waliishi kwa kufuata agano la Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo akamtaka kila mmoja katika Yerusalemu na Benyamini kuweka ahadi zao wenyewe kwa hilo Agano, watu wa Yerusalemu wakafanya hivyo kwa kufuata Agano la BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo akamtaka kila mmoja katika Yerusalemu na Benyamini kuweka ahadi zao wenyewe kwa hilo Agano, watu wa Yerusalemu wakafanya hivyo kwa kufuata Agano la bwana, Mungu wa baba zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawafanya wote walioonekana katika Yerusalemu na Benyamini walikubali. Na wenyeji wa Yerusalemu wakafanya kulingana na agano la Mungu, Mungu wa baba zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena aliwafanya wote waliokuwa katika Yerusalemu na katika Benyamini kuzingatia agano. Nao wakazi wa Yerusalemu waliishi kwa kufuata agano la Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wote walioonekana mle Yerusalemu namo katika nchi ya Benyamini akawashurutisha kulisimamia hilo agano, nao wenyeji wa Yerusalemu wakafanya, kama Agano la Mungu aliye Mungu wa baba zao lilivyowatakia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawafanya wote walioonekana katika Yerusalemu na Benyamini walikubali. Na wenyeji wa Yerusalemu wakafanya sawasawa na agano la Mungu, Mungu wa baba zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tena akawasukuma wote waliokuwa katika Yerusalema na inchi ya Benjamina kushika agano lile. Nao wakaaji wa Yerusalema walitenda kwa kufuata agano la Mungu, Mungu wa babu zao.