2 Chronicles 34:33 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yosia aliondoa sanamu zote za kuchukiza zilizokuwa katika eneo lote la watu wa Israeli, na kuwahimiza watu wote wa Israeli kumtumikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Katika maisha yake yote hawakumwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yosia akaondoa machukizo yote ya sanamu kutoka nchi yote ya Waisraeli na akawataka wale wote waliokuwa katika Israeli wamtumikie Mwenyezi Mungu, Mungu wao. Kwa muda wote alioishi, hawakushindwa kumfuata Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Yosia akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi zote zilizokuwa milki ya wana wa Israeli, akawafanya wote walioonekana katika Israeli kutumika, naam, wamtumikie Bwana, Mungu wao. Siku zake zote hawakuacha kumfuata Bwana, Mungu wa baba zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yosia aliondoa sanamu zote za kuchukiza zilizokuwa katika eneo lote la watu wa Israeli, na kuwahimiza watu wote wa Israeli kumtumikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Katika maisha yake yote hawakumwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yosia akaondoa machukizo yote ya sanamu kutoka katika nchi yote iliyokuwa mali ya Waisraeli na akawataka wale wote waliokuweko katika Israeli wamtumikie BWANA Mungu wao. Kwa muda wote alioishi, hawakushindwa kumfuata BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yosia akaondoa machukizo yote ya sanamu kutoka nchi yote iliyokuwa mali ya Waisraeli na akawataka wale wote waliokuwako katika Israeli wamtumikie bwana Mwenyezi Mungu wao. Kwa muda wote alioishi, hawakushindwa kumfuata bwana, Mungu wa baba zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye Yosia akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi zote zilizokuwa milki ya wana wa Israeli, akawafanya wote walioonekana katika Israeli kutumika, naam, wamtumikie BWANA, Mungu wao. Siku zake zote hawakuacha kumfuata BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yosia aliondoa sanamu zote za kuchukiza zilizokuwa katika eneo lote la watu wa Israeli, na kuwahimiza watu wote wa Israeli kumtumikia Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Katika maisha yake yote hawakumwacha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa babu zao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yosia akaondoa kabisa matambikoi yote yatapishayo katika nchi zote zilizokuwa zao wana wa Isiraeli, nao watu wote walioonekana kwa Waisiraeli akawashurutisha kumtumikia Bwana Mungu wao, nazo siku zake zote za kuwapo hawakuacha kumfuata Bwana Mungu wa baba zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye Yosia akayaondolea mbali machukizo yote katika nchi zote zilizokuwa milki ya wana wa Israeli, akawafanya wote walioonekana katika Israeli kutumika, naam, wamtumikie BWANA, Mungu wao. Siku zake zote hawakuacha kumfuata BWANA, Mungu wa baba zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yosia akaondoa sanamu zote za kuchukiza zilizokuwa katika eneo lote la watu wa Israeli, na kuwasukuma watu wote wa Israeli kumutumikia Yawe, Mungu wao. Katika maisha yake yote hawakumwacha Yawe, Mungu wa babu zao.