2 Chronicles 34:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wake walizibomoa madhabahu za ibada za Mabaali mbele yake na alizikatakata madhabahu za kufukizia ubani zilizoinuliwa juu ya madhabahu hizo; pia alizipondaponda sanamu za Ashera na nyinginezo za kuchonga na za kusubu; alizifanya kuwa mavumbi, nayo mavumbi akayamwaga juu ya makaburi ya wale ambao hapo awali walizitolea sadaka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mbele ya macho yake, wakazibomoa madhabahu za Mabaali, wakazivunja madhabahu za kufukizia uvumba zilizokuwa zimesimama juu yake, wakazivunja nguzo za Ashera, sanamu na vinyago. Hivi alivivunja vipande vipande na kutawanya juu ya makaburi ya waliokuwa wamevitolea sadaka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakazibomoa madhabahu za mabaali machoni pake; na sanamu za jua, zilizoinuliwa juu yake, akazikata-kata; na maashera, na sanamu za kuchonga, nazo za kusubu, akazivunja-vunja, akaziponda kuwa mavumbi, akayamimina juu ya makaburi ya hao waliozichinjia dhabihu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wake walizibomoa madhabahu za ibada za Mabaali mbele yake na alizikatakata madhabahu za kufukizia ubani zilizoinuliwa juu ya madhabahu hizo; pia alizipondaponda sanamu za Ashera na nyinginezo za kuchonga na za kusubu; alizifanya kuwa mavumbi, nayo mavumbi akayamwaga juu ya makaburi ya wale ambao hapo awali walizitolea sadaka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mbele ya macho yake, wakazibomoa madhabahu za Mabaali, wakazivunja madhabahu za kufukizia uvumba zilizokuwa zimesimama juu yake, wakazivunja nguzo za Ashera, sanamu na vinyago. Hivi alivivunja vipande vipande na kuvisambaza juu ya makaburi ya waliokuwa wamevitolea kafara.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mbele ya macho yake, wakazibomoa madhabahu za Mabaali, wakazivunja madhabahu za kufukizia uvumba zilizokuwa zimesimama juu yake, wakazivunja nguzo za Ashera, sanamu na vinyago. Hivi alivivunja vipande vipande na kuvisambaza juu ya makaburi ya waliokuwa wamevitolea kafara.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakazibomoa madhabahu za mabaali machoni pake; na sanamu za jua, zilizoinuliwa juu yake, akazikatakata; Maashera, sanamu za kuchonga, na za kusubu, akazivunjavunja, akaziponda kuwa mavumbi, akayamimina juu ya makaburi ya hao waliozichinjia dhabihu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wake walizibomoa madhabahu za ibada za Mabaali mbele yake na alizikatakata madhabahu za kufukizia ubani zilizoinuliwa juu ya madhabahu hizo; pia alizipondaponda sanamu za Ashera na nyinginezo za kuchonga na za kusubu; alizifanya kuwa mavumbi, nayo mavumbi akayamwaga juu ya makaburi ya wale ambao hapo awali walizitolea sadaka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Usoni pake wakazivunjavunja meza za kuyatambikia Mabaali, nayo mifano ya jua iliyosimamishwa juu yao wakaikatakata, nayo miti ya Ashera na vinyago vingine vya kuchonga navyo vilivyoyeyushwa akavipondaponda, hata vikawa mavumbi, kisha hayo mavumbi akayamwaga juu ya makaburi yao waliovitambikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakazibomoa madhabahu za mabaali machoni pake; na sanamu za jua, zilizoinuliwa juu yake, akazikata-kata; na maashera, na sanamu za kuchonga, nazo za kusubu, akazivunja-vunja, akaziponda kuwa mavumbi, akayamimina juu ya makaburi ya hao waliozichinjia dhabihu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wake walibomoa mazabahu za ibada za Mabali mbele yake na alikatakata mazabahu za kufukizia ubani zilizoinuliwa juu ya mazabahu hizo; vilevile alipondaponda sanamu za Ashera na zingine za kuchonga na za kuyeyusha; akazifanya kuwa mavumbi, nayo mavumbi akayamwanga juu ya makaburi ya wale ambao walizitolea sadaka.