2 Chronicles 35:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo basi, huduma yote ya Mwenyezi-Mungu ilitayarishwa siku hiyo, ili kuiadhimisha Pasaka na kutoa sadaka za kuteketeza kwenye madhabahu ya Mwenyezi-Mungu kama alivyoamuru mfalme Yosia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo wakati ule, huduma yote ya Mwenyezi Mungu ilifanyika katika kuadhimisha Pasaka, na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Mwenyezi Mungu, kama alivyoamuru Mfalme Yosia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi huduma yote ya Bwana ikatengenezwa siku ile ile, kuifanya pasaka, na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana, kama alivyoamuru mfalme Yosia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo basi, huduma yote ya Mwenyezi-Mungu ilitayarishwa siku hiyo, ili kuiadhimisha Pasaka na kutoa sadaka za kuteketeza kwenye madhabahu ya Mwenyezi-Mungu kama alivyoamuru mfalme Yosia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo wakati ule huduma yote ya BWANA ilifanyika katika kuadhimisha Pasaka, kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya BWANA kama alivyoamuru Mfalme Yosia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo wakati ule huduma yote ya bwana ilifanyika katika kuadhimisha Pasaka, kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya bwana kama alivyoamuru Mfalme Yosia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi huduma yote ya BWANA ikatengenezwa siku ile ile, kuifanya Pasaka, na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya BWANA, kama alivyoamuru mfalme Yosia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo basi, huduma yote ya Mwenyezi-Mungu ilitayarishwa siku hiyo, ili kuiadhimisha Pasaka na kutoa sadaka za kuteketeza kwenye madhabahu ya Mwenyezi-Mungu kama alivyoamuru mfalme Yosia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, kazi zote za utumishi wa Bwana zilivyotengenezwa siku ile ya kufanya Pasaka pamoja na kuteketeza ng'ombe za tambiko mezani pa kumtambikia Bwana, kama mfalme Yosia alivyoagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi huduma yote ya BWANA ikatengenezwa siku ile ile, kuifanya pasaka, na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya BWANA, kama alivyoamuru mfalme Yosia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hivyo basi, kazi yote ya Yawe ikatayarishwa siku hiyo, kwa kufanya Pasaka na kutoa sadaka za kuteketeza kwenye mazabahu ya Yawe; kama vile mufalme Yosia alivyoamuru.