2 Chronicles 35:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yosia hakukubali kumwachia. Alikataa kuyasikiliza maneno aliyonena Mungu kwa njia ya Neko, kwa hiyo akajibadilisha ili asitambulike, kisha akaingia vitani katika tambarare ya Megido.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini hata hivyo, Yosia hakukubali kumwacha, bali alijibadilisha ili kupigana naye vita. Hakusikiliza yale Neko aliyokuwa amemwambia kwa agizo la Mungu bali alienda kupigana naye katika tambarare ya Megido.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Walakini Yosia hakukubali kumgeuzia uso mbali, akajibadilisha apate kupigana naye, asiyasikilize maneno ya Neko, yaliyotoka kinywani kwa Mungu, akaja kupigana bondeni mwa Megido.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yosia hakukubali kumwachia. Alikataa kuyasikiliza maneno aliyonena Mungu kwa njia ya Neko, kwa hiyo akajibadilisha ili asitambulike, kisha akaingia vitani katika tambarare ya Megido.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini hata hivyo, Yosia hakukubali kumwacha, bali alijibadilisha ili kupigana naye vita. Hakusikiliza yale Neko aliyokuwa amemwambia kwa agizo la Mungu bali alikwenda kupigana naye katika tambarare ya Megido.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini hata hivyo, Yosia hakukubali kumwacha, bali alijibadilisha ili kupigana naye vita. Hakusikiliza yale Neko aliyokuwa amemwambia kwa agizo la Mungu bali alikwenda kupigana naye katika tambarare ya Megido.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Yosia hakukubali kumwachia, akajibadilisha apate kupigana naye, asiyasikilize maneno ya Neko, yaliyotoka kinywani kwa Mungu, akaja kupigana bondeni mwa Megido.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yosia hakukubali kumwachia. Alikataa kuyasikiliza maneno aliyonena Mungu kwa njia ya Neko, kwa hiyo akajibadilisha ili asitambulike, kisha akaingia vitani katika tambarare ya Megido.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Yosia hakuugeuza uso wake na kumwacha, ila alijipa moyo mwingine kwenda kupigana naye, asiyasikie maneno ya Neko yaliyotoka kinywani mwa Mungu, akaenda kupigana naye bondeni kwa Megido.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Walakini Yosia hakukubali kumgeuzia uso mbali, akajibadilisha apate kupigana naye, asiyasikilize maneno ya Neko, yaliyotoka kinywani kwa Mungu, akaja kupigana bondeni mwa Megido.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yosia hakukubali kumwachilia. Akakataa kusikiliza maneno Mungu aliyosema kwa njia ya Neko, kwa hiyo akajibadilisha kusudi asitambulikane, kisha akaingia katika vita katika bonde la Megido.