2 Chronicles 35:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watumishi wake walimtoa katika gari lake la farasi, wakambeba na gari lake la pili hadi Yerusalemu. Hapo akafariki dunia na kuzikwa katika makaburi ya kifalme. Watu wote wa Yuda na Yerusalemu waliomboleza kifo cha Yosia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo wakamshusha kutoka gari lake la vita, wakamweka kwenye gari lingine alilokuwa nalo na kumleta Yerusalemu, ambako alifia. Akazikwa katika makaburi ya baba zake, nayo Yuda yote na Yerusalemu wakamwombolezea Yosia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi watumishi wake wakamtoa garini, wakamtia katika gari la pili alilokuwa nalo, wakamleta Yerusalemu; naye akafa, akazikwa makaburini mwa babaze. Wakamlilia Yosia Yuda wote na Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watumishi wake walimtoa katika gari lake la farasi, wakambeba na gari lake la pili hadi Yerusalemu. Hapo akafariki dunia na kuzikwa katika makaburi ya kifalme. Watu wote wa Yuda na Yerusalemu waliomboleza kifo cha Yosia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo wakamshusha kutoka kwenye gari lake la farasi, wakamweka kwenye gari lingine alilokuwa nalo na kumleta Yerusalemu, ambako alifia. Akazikwa katika makaburi ya baba zake, nayo Yuda yote na Yerusalemu wakamwombolezea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo wakamshusha kutoka kwenye gari lake la farasi, wakamweka kwenye gari lingine alilokuwa nalo na kumleta Yerusalemu, ambako alifia. Akazikwa katika makaburi ya baba zake, nayo Yuda yote na Yerusalemu wakamwombolezea Yosia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi watumishi wake wakamtoa garini, wakamtia katika gari la pili alilokuwa nalo, wakamleta Yerusalemu; naye akafa, akazikwa makaburini mwa babaze. Watu wote wa Yuda na Yerusalemu wakamlilia Yosia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watumishi wake walimtoa katika gari lake la farasi, wakambeba na gari lake la pili hadi Yerusalemu. Hapo akafariki dunia na kuzikwa katika makaburi ya kifalme. Watu wote wa Yuda na Yerusalemu waliomboleza kifo cha Yosia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watumishi wake walipomtoa katika gari na kumweka katika gari la pili, alilokuwa nalo, wakampeleka Yerusalemu; ndiko, alikokufa. Wakamzika makaburini kwa baba zake. Nao Wayuda na Wayerusalemu wote wakamlilia Yosia,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi watumishi wake wakamtoa garini, wakamtia katika gari la pili alilokuwa nalo, wakamleta Yerusalemu; naye akafa, akazikwa makaburini mwa babaze. Wakamlilia Yosia Yuda wote na Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi watumishi wake walipomutoa katika gari lake la vita, wakamubeba na gari lake la pili mpaka Yerusalema. Naye akakufa na kuzikwa katika makaburi ya kifalme. Watu wote wa inchi ya Yuda na Yerusalema wakaomboleza kifo cha Yosia.