2 Chronicles 35:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Pamoja na hayo, aliwapa Walawi waliowafundisha watu wa Israeli na ambao walikuwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, maagizo yafuatayo: “Liwekeni sanduku takatifu ndani ya nyumba ambayo Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli alijenga; hamhitaji kulibebabeba tena mabegani. Sasa mtumikieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na watu wake Waisraeli.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akawaambia Walawi, waliowafundisha Waisraeli wote na waliokuwa wamejiweka wakfu kwa ajili ya kazi ya Mwenyezi Mungu, “Liwekeni hilo Sanduku takatifu katika Hekalu lile alilojenga Sulemani mwana wa Daudi mfalme wa Israeli. Halipaswi kubebwa mabegani mwenu. Sasa mtumikieni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na watu wake Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaambia Walawi, waliowafundisha Israeli wote, waliotakasika kwa Bwana, Wekeni sanduku takatifu katika nyumba aliyoijenga Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli; hamtakuwa tena na mzigo mabegani; sasa mtumikieni Bwana, Mungu wenu, na watu wake Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Pamoja na hayo, aliwapa Walawi waliowafundisha watu wa Israeli na ambao walikuwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, maagizo yafuatayo: “Liwekeni sanduku takatifu ndani ya nyumba ambayo Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli alijenga; hamhitaji kulibebabeba tena mabegani. Sasa mtumikieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na watu wake Waisraeli.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akawaambia Walawi, waliowafundisha Waisraeli wote na ambao walikuwa wamejiweka wakfu kwa ajili ya kazi ya BWANA, “Liwekeni hilo Sanduku takatifu katika Hekalu lile alilojenga Solomoni mwana wa Daudi mfalme wa Israeli. Halipaswi kubebwa huko na huko mabegani mwenu. Sasa mtumikieni BWANA Mungu wenu na watu wake Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akawaambia Walawi, waliowafundisha Waisraeli wote na waliokuwa wamejiweka wakfu kwa ajili ya kazi ya bwana, “Liwekeni hilo Sanduku takatifu katika Hekalu lile alilojenga Sulemani mwana wa Daudi mfalme wa Israeli. Halipaswi kubebwa huku na huko mabegani mwenu. Sasa mtumikieni bwana Mwenyezi Mungu wenu na watu wake Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaambia Walawi, waliowafundisha Israeli wote, waliotakasika kwa BWANA, Wekeni sanduku takatifu katika nyumba aliyoijenga Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli; hamtakuwa tena na mzigo mabegani; sasa mtumikieni BWANA, Mungu wenu, na watu wake Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Pamoja na hayo, aliwapa Walawi waliowafundisha watu wa Israeli na ambao walikuwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, maagizo yafuatayo: “Liwekeni sanduku takatifu ndani ya nyumba ambayo Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli alijenga; hamhitaji kulibebabeba tena mabegani. Sasa mtumikieni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu na watu wake Waisraeli.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawaambia Walawi waliowafundisha Waisiraeli wote, waliokuwa watakatifu wa Bwana: Liwekeni Sanduku takatifu katika hiyo Nyumba, aliyoijenga Salomo, mwana wa Dawidi, mfalme wa Waisiraeli! Msilichukue tena mabegani! Sasa mtumikieni Bwana Mungu wenu, mwatumikie nao walio ukoo wake,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaambia Walawi, waliowafundisha Israeli wote, waliotakasika kwa BWANA, Wekeni sanduku takatifu katika nyumba aliyoijenga Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli; hamtakuwa tena na mzigo mabegani; sasa mtumikieni BWANA, Mungu wenu, na watu wake Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pamoja na hayo, akawapa Walawi waliowafundisha watu wa Israeli na ambao walitakaswa kwa ajili ya Yawe, maagizo haya: “Muweke Sanduku takatifu ndani ya nyumba ambayo Solomono mwana wa Daudi, mufalme wa Israeli aliyojenga; hamuhitaji kulibebabeba tena juu ya mabega. Sasa mumutumikie Yawe, Mungu wenu, na watu wake Waisraeli.