2 Chronicles 35:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Yosia aliwapa watu, wanambuzi wapatao 30,000, na mafahali 3,000, wote hawa walitolewa kwenye mifugo ya mfalme.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Yosia akawapa watu wote waliokuwepo wana-mbuzi na kondoo wapatao elfu thelathini kwa ajili ya sadaka ya Pasaka, pia na ng’ombe elfu kumi; wote kutoka kwa mali binafsi ya mfalme.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena Yosia akawapa wana wa watu, matoleo ya makundi, wana-kondoo na wana-mbuzi, yote yawe kwa ajili ya matoleo ya pasaka, wote waliokuwako, wakipata thelathini elfu, na ng'ombe elfu tatu; hao walitoka katika mali za mfalme.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Yosia aliwapa watu, wanambuzi wapatao 30,000, na mafahali 3,000, wote hawa walitolewa kwenye mifugo ya mfalme.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yosia akawapa watu wote wana-mbuzi waliokuwepo jumla ya kondoo wapatao 30,000 kwa ajili ya sadaka ya Pasaka, pia na ng'ombe 10,000, vyote hivi kutoka katika mali binafsi ya mfalme.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Yosia akawapa watu wote wana-mbuzi waliokuwepo jumla ya kondoo wapatao 30,000 kwa ajili ya sadaka ya Pasaka, pia na ng’ombe 10,000, vyote hivi kutoka mali binafsi ya mfalme.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena Yosia akawapa watu, matoleo ya makundi, wana-kondoo na wana-mbuzi, yote yawe kwa ajili ya matoleo ya Pasaka, wote waliokuwako, wakiwa elfu thelathini, na ng'ombe elfu tatu; hao walitoka katika mali za mfalme.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Yosia aliwapa watu, wanambuzi wapatao 30,000, na mafahali 3,000, wote hawa walitolewa kwenye mifugo ya mfalme.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha mfalme akawatolea watu kondoo na wana mbuzi, wote kuwa wa Pasaka wa watu wote waliooneka, wote wakawa 30000 na ng'ombe 3000, wote walitoka katika makundi ya mfalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena Yosia akawapa wana wa watu, matoleo ya makundi, wana-kondoo na wana-mbuzi, yote yawe kwa ajili ya matoleo ya pasaka, wote waliokuwako, wakipata thelathini elfu, na ng’ombe elfu tatu; hao walitoka katika mali za mfalme.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yosia akawapa watu, wana-mbuzi yapata elfu makumi tatu, na ngombe dume elfu tatu, wote hawa toka katika makundi ya mufalme.