2 Chronicles 36:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwaka ulipokwisha, mfalme Nebukadneza alituma wajumbe, wakamchukua Yehoyakini mateka hadi Babuloni, pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Akamtawaza Sedekia, nduguye, kuwa mfalme wa Yuda na Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Majira ya vuli, Mfalme Nebukadneza akatuma watu, nao wakamleta Babeli, pamoja na vyombo vya thamani kutoka Hekalu la Mwenyezi Mungu. Naye akamfanya Sedekia, ndugu yake Yehoyakimu kuwa mfalme wa Yuda na Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwaka ulipokwisha, Nebukadreza akatuma wajumbe, akamchukua mpaka Babeli; pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya Bwana; akamtawaza Sedekia nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwaka ulipokwisha, mfalme Nebukadneza alituma wajumbe, wakamchukua Yehoyakini mateka hadi Babuloni, pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Akamtawaza Sedekia, nduguye, kuwa mfalme wa Yuda na Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mnamo majira ya vuli, Mfalme Nebukadneza akatuma watu wakamleta Babeli, pamoja na vyombo vya thamani kutoka katika Hekalu la BWANA naye akamfanya Sedekia, ndugu yake Yehoyakimu kuwa mfalme wa Yuda na Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mnamo majira ya vuli, Mfalme Nebukadneza akatuma watu, nao wakamleta Babeli, pamoja na vyombo vya thamani kutoka Hekalu la bwana. Naye akamfanya Sedekia, ndugu yake Yehoyakimu kuwa mfalme wa Yuda na Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwaka ulipokwisha, Nebukadneza akatuma wajumbe, akamchukua mpaka Babeli; pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya BWANA; akamtawaza Sedekia nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwaka ulipokwisha, mfalme Nebukadneza alituma wajumbe, wakamchukua Yehoyakini mateka hadi Babuloni, pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Akamtawaza Sedekia, nduguye, kuwa mfalme wa Yuda na Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwaka mwingine ulipoanza, mfalme Nebukadinesari akatuma, akampeleka Babeli pamoja na vyombo vya Nyumba ya Bwana, alivyovitamani, akamfanya ndugu yake Sedekia kuwa mfalme wao Wayuda na Wayerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwaka ulipokwisha, Nebukadreza akatuma wajumbe, akamchukua mpaka Babeli; pamoja na vyombo vya thamani vya nyumba ya BWANA; akamtawaza Sedekia nduguye awe mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mwaka ulipokwisha, mufalme Nebukadneza alituma wajumbe, wakamuchukua Yoyakini na kumupeleka mpaka Babeli, pamoja na vyombo vya bei kali vya nyumba ya Yawe. Akamweka ndugu yake Sedekia kuwa mufalme wa Yuda na Yerusalema.