2 Chronicles 36:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata makuhani, viongozi wa Yuda pamoja na watu walikosa uaminifu kabisa wakiiga matendo yote ya kuchukiza ya watu wa mataifa mengine; waliichafua nyumba ya Mwenyezi-Mungu ambayo yeye mwenyewe alikuwa ameitakasa huko Yerusalemu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Zaidi ya hayo viongozi wote wa makuhani pamoja na watu wakazidi kukosa uaminifu zaidi na zaidi, wakafanya machukizo yote kama walivyofanya mataifa wakinajisi Hekalu la Mwenyezi Mungu alilokuwa amelitakasa huko Yerusalemu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya Bwana aliyoitakasa katika Yerusalemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata makuhani, viongozi wa Yuda pamoja na watu walikosa uaminifu kabisa wakiiga matendo yote ya kuchukiza ya watu wa mataifa mengine; waliichafua nyumba ya Mwenyezi-Mungu ambayo yeye mwenyewe alikuwa ameitakasa huko Yerusalemu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Zaidi ya hayo viongozi wote wa makuhani pamoja na watu wakazidi kukosa uaminifu zaidi na zaidi, wakafanya machukizo yote kama walivyofanya mataifa wakinajisi Hekalu la BWANA alilokuwa amelitakasa huko Yerusalemu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Zaidi ya hayo viongozi wote wa makuhani pamoja na watu wakazidi kukosa uaminifu zaidi na zaidi, wakafanya machukizo yote kama walivyofanya mataifa wakinajisi Hekalu la bwana alilokuwa amelitakasa huko Yerusalemu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno wakifuata machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA aliyoitakasa katika Yerusalemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata makuhani, viongozi wa Yuda pamoja na watu walikosa uaminifu kabisa wakiiga matendo yote ya kuchukiza ya watu wa mataifa mengine; waliichafua nyumba ya Mwenyezi-Mungu ambayo yeye mwenyewe alikuwa ameitakasa huko Yerusalemu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wakuu wote wa watambikaji na wa watu wakazidi kuyavunja maagano na kufanya mengi kama hayo matapisho yote ya wamizimu, hata Nyumba ya Bwana wakaichafua, aliyoitakasa mle Yerusalemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na zaidi ya hayo wakuu wote wa makuhani, na watu, wakakosa mno sawasawa na machukizo yote ya mataifa; wakainajisi nyumba ya BWANA aliyoitakasa katika Yerusalemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata makuhani, viongozi wa inchi ya Yuda pamoja na watu walikosa uaminifu kabisa wakiiga matendo yote ya kuchukiza ya watu wa mataifa mengine; waliichafua nyumba ya Yawe ambayo yeye mwenyewe alikuwa ameitakasa kule Yerusalema.