2 Chronicles 36:22 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi, mfalme wa Persia, ili litimie neno la Mwenyezi-Mungu alilolinena kwa njia ya nabii Yeremia, Mwenyezi-Mungu alimfanya Koreshi, mfalme wa Persia, atangaze amri ifuatayo katika ufalme wake wote na kuiweka katika maandishi:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kulitimiza neno la Mwenyezi Mungu lililosemwa na nabii Yeremia, Mwenyezi Mungu aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote kwa maandishi:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi, mfalme wa Persia, ili litimie neno la Mwenyezi-Mungu alilolinena kwa njia ya nabii Yeremia, Mwenyezi-Mungu alimfanya Koreshi, mfalme wa Persia, atangaze amri ifuatayo katika ufalme wake wote na kuiweka katika maandishi:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili litimie lile neno la BWANA lililosemwa na nabii Yeremia, BWANA akausukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutoa tangazo kwa maandishi katika utawala wake wote:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ili kulitimiza neno la bwana lililosemwa na nabii Yeremia, bwana aliusukuma moyo wa Koreshi mfalme wa Uajemi kutangaza katika himaya yake yote kwa maandishi:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo mwaka wa kwanza wa utawala wa Koreshi, mfalme wa Persia, ili litimie neno la Mwenyezi-Mungu alilolinena kwa njia ya nabii Yeremia, Mwenyezi-Mungu alimfanya Koreshi, mfalme wa Persia, atangaze amri ifuatayo katika ufalme wake wote na kuiweka katika maandishi:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa kwanza wa Kiro, mfalme wa Wapersia, ndipo, lilipotimia neno la Bwana, alilolisema kinywani mwa Yeremia, maana Bwana akaiamsha roho yake Kiro, mfalme wa Wapersia, akatangaza mbiu katika ufalme wake wote kwa vinywa vya watu na kwa barua kwamba:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la BWANA alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, BWANA akamwamsha roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia, akisema,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Kiro mufalme wa Persia, kusudi litimie neno la Yawe alilolisema kwa njia ya nabii Yeremia, Yawe aliamusha nia ya Kiro naye akatoa amri hii katika ufalme wake wote, vilevile alituma habari hizo kwa njia ya maandiko: