2 Chronicles 36:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, akatawala kwa muda wa miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu. Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na moja. Akafanya maovu machoni pa Mwenyezi Mungu, Mungu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja; akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, Mungu wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, akatawala kwa muda wa miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu. Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu kwa miaka kumi na mmoja. Akafanya maovu machoni pa BWANA Mungu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, naye akatawala huko Yerusalemu miaka kumi na mmoja. Akafanya maovu machoni pa bwana Mwenyezi Mungu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja; akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, Mungu wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, akatawala kwa muda wa miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu. Alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yoyakimu alikuwa mwenye miaka 25 alipoupata ufalme, akawa mfalme miaka 11 mle Yerusalemu, akayafanya yaliyo mabaya machoni pake Bwana Mungu wake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na mmoja; akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, Mungu wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yoyakimu alikuwa na umri wa miaka makumi mbili na mitano alipoanza kutawala, akatawala kwa muda wa miaka kumi na mumoja akiwa kule Yerusalema. Alitenda maovu mbele ya Yawe, Mungu wake.