2 Chronicles 4:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Uzani wa shaba iliyotumika kutengenezea vyombo hivi haukujulikana kwa maana Solomoni alitengeneza vyombo vingi sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vitu hivi vyote Mfalme Sulemani alivyotengeneza vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzani wa shaba haungekadirika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndivyo alivyovifanya Sulemani vyombo hivyo vyote, vingi sana; kwa kuwa uzani wa shaba ulikuwa hautafutikani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Uzani wa shaba iliyotumika kutengenezea vyombo hivi haukujulikana kwa maana Solomoni alitengeneza vyombo vingi sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vitu hivi vyote Mfalme Solomoni alivyotengeneza vilikuwa vingi sana kwamba uzito wa shaba haukuweza kuonyeshwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vitu hivi vyote Mfalme Sulemani alivyotengeneza vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzito wa shaba haungekadirika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndivyo Sulemani alivyovitengeneza vyombo hivi vikiwa vingi sana, uzani wa shaba lliyotumika haukujulikana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Uzani wa shaba iliyotumika kutengenezea vyombo hivi haukujulikana kwa maana Solomoni alitengeneza vyombo vingi sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Salomo akavitengeneza hivi vyote kuwa vingi mno, kwani shaba zilizotumika hazikupimwa, wala hazikuulizwa, kama ni ngapi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndivyo alivyovifanya Sulemani vyombo hivyo vyote, vingi sana; kwa kuwa uzani wa shaba ulikuwa hautafutikani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Uzito wa shaba iliyotumiwa kwa kutengeneza vyombo hivi haukujulikana kwa maana Solomono alitengeneza vyombo vingi sana.