2 Chronicles 4:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Unene wa ukingo wake ulikuwa sentimita 7.5. Ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, na kama ua la yungiyungi. Tangi hilo liliweza kuchukua kiasi cha lita 60,000 za maji.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Unene wake ulikuwa nyanda moja, na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Ingejazwa na bathi elfu tatu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu tatu, kukaa ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Unene wa ukingo wake ulikuwa sentimita 7.5. Ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, na kama ua la yungiyungi. Tangi hilo liliweza kuchukua kiasi cha lita 60,000 za maji.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Unene wake ulikuwa nyanda nne, ambao ulikuwa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi li lililochanua. Bahari hii iliweza kuchukua kiasi cha bathi 3,000.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Iliweza kuchukua bathi 3,000.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu tatu, kukaa ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Unene wa ukingo wake ulikuwa sentimita 7.5. Ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, na kama ua la yungiyungi. Tangi hilo liliweza kuchukua kiasi cha lita 60,000 za maji.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Unene wake ulikuwa upana wa shibiri, nao ukingo wake wa juu ulikuwa kama wa kikombe au kama wa ua la uwago. Ndani yake zikaenea bati 3000, ndio pishi 27000.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu tatu, kukaa ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Unene wa ukingo wake ulikuwa sentimetre saba na nusu. Ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, na kama maua ya yungiyungi. Ndani ya birika lile kuliweza kuingia kadiri ya litre elfu makumi sita za maji.