2 Chronicles 4:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alitengeneza pia birika kumi za kuoshea vitu vilivyotumika katika tambiko za kuteketezwa. Tano kati ya bakuli hizo aliziweka kusini na tano upande wa kaskazini. Tangi lilitumiwa na makuhani kunawia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akatengeneza masinia kumi kwa ajili ya kuoshea vifaa, naye akayaweka matano upande wa kusini na matano upande wa kaskazini. Ndani yake ndimo walioshea vifaa vya kutumika katika sadaka za kuteketezwa, lakini ile Bahari ilikuwa ya makuhani kunawia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kuume, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alitengeneza pia birika kumi za kuoshea vitu vilivyotumika katika tambiko za kuteketezwa. Tano kati ya bakuli hizo aliziweka kusini na tano upande wa kaskazini. Tangi lilitumiwa na makuhani kunawia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akatengeneza masinia kumi kwa ajili ya kuoshea vifaa, naye akayaweka matano upande wa kusini na matano upande wa kaskazini. Ndani yake ndimo vilimooshewa vifaa vya kutumika katika sadaka za kuteketezwa, lakini ile Bahari ilikuwa ni kwa ajili ya makuhani kunawia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akatengeneza masinia kumi kwa ajili ya kuoshea vifaa, naye akayaweka matano upande wa kusini na matano upande wa kaskazini. Ndani yake ndimo walioshea vifaa vya kutumika katika sadaka za kuteketezwa, lakini ile Bahari ilikuwa ni kwa ajili ya makuhani kunawia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alitengeneza pia birika kumi za kuoshea vitu vilivyotumika katika tambiko za kuteketezwa. Tano kati ya bakuli hizo aliziweka kusini na tano upande wa kaskazini. Tangi lilitumiwa na makuhani kunawia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akatengeneza hata mitungi 10 ya kuoshea, mitano akaweka kuumeni, mitano kushotoni; ndimo, walimosafishia vyombo vilivyotumika katika kazi za kuteketeza ng'ombe za tambiko, lakini bahari ilikuwa yao watambikaji ya kuogea.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kuume, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akatengeneza vilevile beseni kumi za kusafishia sehemu za nyama zilizotumika katika sadaka za kuteketezwa kwa moto. Tano kati ya bakuli zile akaziweka upande wa kusini na tano upande wa kaskazini. Birika lilitumiwa na makuhani kwa kunawia.