2 Chronicles 4:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alitengeneza vinara kumi vya dhahabu kama ilivyoagizwa, akaviweka ukumbini mwa hekalu; vitano upande wa kusini, na vitano upande wa kaskazini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akatengeneza vinara kumi vya taa vya dhahabu kama ilivyoainishwa na kuviweka hekaluni, vinara vitano upande wa kusini, na vitano upande wa kaskazini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akavifanya vinara vya taa kumi vya dhahabu, kadiri ya vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kuume, na vitano upande wa kushoto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alitengeneza vinara kumi vya dhahabu kama ilivyoagizwa, akaviweka ukumbini mwa hekalu; vitano upande wa kusini, na vitano upande wa kaskazini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akatengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu kama ilivyoainishwa kwao na kuviweka hekaluni, vinara vitano upande wa kusini na vitano upande wa kaskazini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akatengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu kama ilivyoainishwa kwao na kuviweka hekaluni, vinara vitano upande wa kusini na vitano upande wa kaskazini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alivitengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu, kama vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kulia, na vitano upande wa kushoto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alitengeneza vinara kumi vya dhahabu kama ilivyoagizwa, akaviweka ukumbini mwa hekalu; vitano upande wa kusini, na vitano upande wa kaskazini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akatengeneza hata vinara 10 vya dhahabu sawasawa, kama ilivyoagizwa kuvitengeneza, akaviweka mle jumbani vitano kuumeni, vitano kushotoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akavifanya vinara vya taa kumi vya dhahabu, kadiri ya vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kuume, na vitano upande wa kushoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alitengeneza vinara kumi vya zahabu kama vile ilivyoagizwa, akaviweka katika baraza ya hekalu; vitano upande wa kusini, na vitano upande wa kaskazini.