2 Chronicles 5:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo, Solomoni akamaliza kazi zote zilizohusu nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Kisha Solomoni akaleta mali yote Daudi baba yake aliyokuwa ameiweka wakfu, yaani: Fedha, dhahabu na vyombo; akaiweka katika hazina za nyumba ya Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Sulemani alipomaliza kazi ya Hekalu la Mwenyezi Mungu, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: yaani fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hivyo ikaisha kazi yote Sulemani aliyoifanyia nyumba ya Bwana. Sulemani akaviingiza vitu alivyovitakasa baba yake Daudi; fedha, na dhahabu, na vyombo vyote, akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Mungu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo, Solomoni akamaliza kazi zote zilizohusu nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Kisha Solomoni akaleta mali yote Daudi baba yake aliyokuwa ameiweka wakfu, yaani: fedha, dhahabu na vyombo; akaiweka katika hazina za nyumba ya Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo kazi yote Solomoni aliyofanya kwa ajili ya Hekalu la BWANA ikamalizika, Solomoni akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu, yaani, fedha, dhahabu na vyombo vingine vyote na kuviweka katika hazina za Hekalu la Mungu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo Sulemani alipomaliza kazi ya Hekalu la bwana, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: yaani, fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Mungu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hivyo ikaisha kazi yote Sulemani aliyoifanyia nyumba ya BWANA. Sulemani akaviingiza vitu alivyovitakasa baba yake Daudi; fedha, na dhahabu, na vyombo vyote, akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo, Solomoni akamaliza kazi zote zilizohusu nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Kisha Solomoni akaleta mali yote Daudi baba yake aliyokuwa ameiweka wakfu, yaani: Fedha, dhahabu na vyombo; akaiweka katika hazina za nyumba ya Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kazi zote, ambazo Salomo aliifanyia nyumba ya Bwana zilipomalizika, Salomo akavipeleka vipaji vitakatifu vyote vya baba yake Dawidi pamoja na fedha na dhahabu na vyombo vyote, akaviweka penye vilimbiko vya nyumba ya Mungu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hivyo ikaisha kazi yote Sulemani aliyoifanyia nyumba ya BWANA. Sulemani akaviingiza vitu alivyovitakasa baba yake Daudi; fedha, na dhahabu, na vyombo vyote, akavitia ndani ya hazina za nyumba ya Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Solomono akamaliza kazi zote zilizoelekea nyumba ya Yawe. Kisha Solomono akaleta mali yote baba yake Daudi aliyokuwa ameitoa kwa Mungu, ni kusema: feza, zahabu na vyombo; akaiweka katika hazina za nyumba ya Mungu.