2 Chronicles 5:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hakukuwa na kitu ndani ya sanduku la agano, ila vile vibao viwili vya mawe ambavyo Mose aliviweka humo kule Horebu, mahali Mwenyezi-Mungu alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndani ya Sanduku hapakuwa na kitu kingine chochote isipokuwa vile vibao viwili ambavyo Musa aliviweka ndani yake huko Horebu, mahali Mwenyezi Mungu alipofanya agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili alizozitia Musa huko Horebu, Bwana alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hakukuwa na kitu ndani ya sanduku la agano, ila vile vibao viwili vya mawe ambavyo Mose aliviweka humo kule Horebu, mahali Mwenyezi-Mungu alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine cho chote isipokuwa zile mbao mbili ambazo Mose alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali BWANA alipofanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine chochote isipokuwa zile mbao mbili ambazo Musa alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali ambapo bwana alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili alizozitia Musa huko Horebu, BWANA alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hakukuwa na kitu ndani ya sanduku la agano, ila vile vibao viwili vya mawe ambavyo Mose aliviweka humo kule Horebu, mahali Mwenyezi-Mungu alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mle Sandukuni hamkuwamo na kitu, ni zile mbao mbili tu, Mose alizozitia huko Horebu, Bwana alipofanya Agano na wana wa Isiraeli, walipotoka Misri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili alizozitia Musa huko Horebu, BWANA alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ndani ya Sanduku la Agano, hamukukuwa kitu kingine isipokuwa tu vile vibao viwili ambavyo Musa aliviweka mule kule Horebu, pahali Yawe alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka Misri.